KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 11, 2009

Kipa wa Ujerumani 'ajiuwa'


Kipa wa Ujerumani na Hannover 96 Robert Enke amefariki dunia baada ya kugongwa na treni kwa kile kilichothibitishwa na polisi kuwa ni kujiuwa.
Enke, 32, aliuawa kaskazini magharibi mwa mji wa Hannover.

Chama cha soka cha Ujerumani (DFB) kimesema katika taarifa kwamba: "Timu ya Ujerumani imesikitishwa sana na kifo cha Robert Enke."

Meneja wa timu ya ujerumani Oliver Bierhoff aliongeza: "Tumeshtushwa sana.Hatujui tuseme nini."

Aliwahi kuchezea Ujerumani mara nane na pia vilabu vya Carl Zeiss Jena, Borussia Mönchengladbach, Benfica, Barcelona, Fenerbahce na Tenerife, kabla ya kurudi ligi ya Bundesliga akiwa na Hannover mwaka 2004.

No comments:

Post a Comment