KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, November 11, 2009
Jenerali Kazini auawa Kampala
Aliyewahi kuwa kamanda wa majeshi ya Uganda, Jenerali James Kazini ameuawa akiwa nyumbani kwa rafiki yake wa kike mjini Kampala.
Taarifa zinaeleza kuwa Jenerali Kazini alikufa baada ya kupigwa nondo kichwani katika ugomvi baina yao. Rafiki huyo wa kike amekamatwa.
Msemaji wa jeshi ameeleza kuwa Jenerali Kazini alipoteza maisha kutokana na ugomvi wa nyumbani.
James Kazini aliongoza majeshi ya Uganda kuanzia mwaka 2001 kabla ya kutimuliwa mwaka 2003 baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kumshutumu kwa kutorosha maliasili za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati akisimamia operesheni za kijeshi.
Aliwahi kufungwa jela kwa makosa ya rushwa mwaka 2008 na wakati wa kifo chake alikuwa akikabiliwa na mashtaka zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment