KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 25, 2009

FIFA yajikuna kichwa kuhusu kashfa


Shirikisho la kandanda duniani, Fifa, linaandaa mkutano maalum mwezi ujao kujadili matukio mbalimbali ambayo yameghubika ulimwengu wa soka mnamo siku au wiki chache zilizopita.
Hoja kubwa ni kashfa ambazo zimekumba baadhi ya mechi za kufuzu kwa fainali za kombe la dunia.

Kwa wiki nzima sasa mshambuliaji Thierry Henry ametupiwa tope na lawama kuushika mpira na kutoa pasi kwa mwenzake, William Gallas ambaye alifunga bao la ushindi kati ya Ufaransa na Ireland.

Fifa imekataa ombi la Ireland kwamba mechi hiyo ichezwe upya.

Huenda Fifa wakajadili pia kiini cha ghasia na mkwaruzano kati ya Algeria na Misri.

Algeria iliitandika Misri bao 1-0 katika mechi iliyochezewa nchini Sudan kuamua nani atakwenda Afrika Kusini mwaka ujao.

Kwenye ajenda ya shirikisho hilo pia ni vitendo vya kutumia kamari kwa nia ya kushawishi matokeo ya mechi barani ulaya.

Isitoshe, shirika la kandanda la Iraq lilisimamishwa kwa muda kutokana na serikali kuingilia shughuli zake, kinyume na kanuni za Fifa.

No comments:

Post a Comment