Mmarekani mmoja analishitaki shirika la upelelezi la Marekani, FBI baada ya kutotendewa vyema alipokuwa ametiwa gerezani nchini Kenya na Ethiopia mwaka 2007.
Amir Meshal alikamatwa kwenye mpaka wa Kenya alipokimbia kutoka Somalia baada ya uongozi wa kiislam kufutwa.
Kutokana na mashitaka hayo, wapelelezi hao walimsaili akiwa katika nchi hizo wakisema alipata mafunzo kutoka kundi la al-Qaeda nchini Somalia.
Meshal amesema baada ya hapo alirejeshwa Somalia na kupelekwa Ethiopia kwa miezi mitatu ambapo wapelelezi wa Marekani walimtishia kumtesa na kumwuua.
No comments:
Post a Comment