KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, November 18, 2009
EU kuanza kuisaidia Somalia
Muungano wa Ulaya utaanza matayarisho ya kutoa mafunzo nchini Uganda kwa wanajeshi 2,000 wa Somalia.
Uamuzi huo ulipitishwa katika mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa nchi za Ulaya uliofanyika mjini Brussels ni sehemu ya juhudi za kimataifa kuisaidia nchi hiyo inayokumbwa na vita kukabiliana na waasi wa Kiislamu na magenge ya kiharamia.
Muungano wa Ulaya unakusudia kuisaidia serikali dhaifu ya Somalia kuwafunza waliokua wanamgambo kuwa jeshi kamili la askari takriban elfu 6. Askari hao 2,000 kati ya hao watapewa mafunzo na wakufunzi 200 wa muungano wa Ulaya nchini Uganda inayoongoza jeshi la kimataifa la kulinda amani nchini Somalia.
Mataifa kadhaa ikiwemo Ujerumani na Hispania ziko tayari kuchangia mpango huo. Ufaransa tayari inatoa mafunzo kwa wanajeshi 500 wa Somalia katika kituo chao cha kijeshi Djibouti.
Lakini kuna wasiwasi EU inaweza kurudia makosa yale yale iliyoyafanya Afghanistan ambako ina matatizo ya kuwapata wakufunzi wa kutosha wa polisi na kuhakikisha utiifu wa vikosi vya kienyeji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment