KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, November 4, 2009
Congo yakerwa na UN kuinyima msaada
Congo yakerwa na UN kuinyima msaada
Umoja wa mataifa, umekemewa na serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa kusitisha msaada kwa wanajeshi wa serikali wanaopambana dhidi ya makundi ya waasi.
Waziri wa habari na mawasiliano Lambert Mende amefahamisha BBC kwamba hana ufahamu wowote kuhusu mauaji yanayodaiwa na umoja huo kutekelezwa na jeshi la serikali.
Hiyo ndio sababu imepelekea umoja huo kusitisha msaada kwa jeshi la serikali.
Umoja wa mataifa umedai kuwa watu sitini na wawili waliuawa na jeshi la Congo huku mashirika ya kijamii yakituhumu jeshi hilo kwa kuwabaka na kuwaua wanawake.
Waasi hao wa kihutu walitoroka Rwanda mwaka 1994 baada ya kushutumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment