KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, November 17, 2009

Afrika lazima ikomae kiuchumi


Mataifa mengi ya kiafrika ni madogo mno kuweza kujiendeleza binafsi, mfanyabiashara maarufu mzaliwa wa Sudan, Mo Ibrahim ameuambia mkutano uliofanyika Tanzania.
Bw Ibrahim amesema wazo la nchi ndogo 53 za kiafrika kuweza kushindana na China, India, Ulaya na Marekani ni hoja ya kupotosha.

Biashara ndani ya Afrika ni asilimia 4 hadi 5 ya biashara ya kimataifa barani humo, jambo lisiloweza kuleta mafanikio.

Tajiri huyo mkubwa amesema Afrika inahitaji marekebisho ili kushindana na nchi zenye uchumi uliokomaa zaidi.

Mwandishi wa BBC aliyopo Nairobi Peter Greste amesema Bw Ibrahim alikuwa akimaanisha nchi zishirikiane kiuchumi badala ya kuungana kisiasa.

No comments:

Post a Comment