KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 26, 2009

Uamuzi watolewa Sierra Leone


Mahakama inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa nchini Sierra Leone ina mpango wa kukabidhi uamuzi wake wa mwisho juu ya washukiwa wa uhalifu wa kivita.
Uhalifu huo ulitokana na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyotokea nchini humo yaliyomalizika mwaka 2002.

Mgogoro huo ulijaa mauaji, kukatwa viungo vya mwili na uteswaji wa raia.

Viongozi watatu wa waasi watasikia matokeo ya rufaa dhidi ya kutiwa kwao hatiani.

Kesi iliyobaki ni ile ya aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor, ambapo inaendelea kusikilizwa katika mahakama maalum huko the Hague.

No comments:

Post a Comment