KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, October 26, 2009

Rais Tunisia achaguliwa mara ya tano


Kiongozi wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali amechaguliwa tena kwa kura nyingi kuingoza nchi hiyo ambapo amepata asilimia 90 ya kura.
Takwimu rasmi zimeonesha asilimia 84 ya watu waliojiandikisha walipiga kura ya Urais na Wabunge.

Rais huyo mteule atashika madaraka kwa kipindi cha miaka mitano mingine.

Mkuu wa waangalizi wa Muungano wa Afrika, Benjamin Boungolous, ameuelezea uchaguzi huo wa siku ya Jumapili ulikuwa huru na wa haki, lakini hata hivyo upande wa upinzani umesema kulikuwa na kasoro.

Wamesema hakukuwa na uhuru wa kuchagua wakati wa kupiga kura.

Chama tawala cha Rais cha Constitutional Democratic Rally, pia kimezoa viti vingi vya Bunge.

No comments:

Post a Comment