KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 14, 2009

Mashambulio ya waasi yaenea Kongo


Shirika la madaktari lisilokuwa na mipaka limesema hali huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo kundi la waasi la Lord's Resistance Army, LRA hufanyia shughuli zake linazidi kuwa mbaya.
Shirika hilo la Medecins Sans Frontieres limeiambia BBC maelfu ya watu wanakimbia mashambulio mapya ya waasi.

Hapo awali kiongozi wa LRA, Joseph Kony alikuwa akifanyia shughuli zake nchini Uganda lakini wapiganaji wake kwa sasa wameenea sehemu kubwa ya Afrika ya Kati.

Wachambuzi wanasema jaribio lililofanywa na majeshi ya eneo la Afrika ya Kati mwaka huu ya kusimamisha mashambulio hayo hayajafanikiwa.

No comments:

Post a Comment