KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 16, 2009

Kumbukumbu ya Franco


Idhaa ya Kiswahili ya BBC ilifanya vipindi mbali mbali vya kukumbuka miaka 20 tangu kifo cha hayati Luambo Makiadi, a.k.a Franco, mwanamuziki maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.




Siku ya kwanza: Oktoba 05

Swali : Je jina alilopewa Franco alipozaliwa ni lipi na maisha yake ya ujana aliishi wapi ?

Jibu: Francois Lokanga la Djo Pene Luambo Makiadi. Aliishi mtaa wa Kasa Vubu mjini Kinshasa

Mshindi: Hakuna mshindi.

Siku ya pili: Oktoba 06

Swali: Je, Ni nani aliyekuwa mshirika mkubwa wa Franco katika fani ya muziki ?

Jibu : Lutumba Simaro

Mshindi: Deo Asanta kutoka Moshi, Tanzania

Siku ya tatu: Oktoba 07



Dada wa Franco, Marie Jane, kama tulivyomkuta mjini Kinshasa.


Swali: Je, ni nyimbo zipi zilizomtia Franco matatani hadi akafungwa jela?

Jibu: Helene, Jacky na Francois

Mshindi: Hakuna Mshindi

Siku ya nne: Oktoba 08

Swali: Je mwezi huu wa Oktoba mwaka 1971, Franco Luambo Makiadi alitoa tangazo lipi la kihistoria kupitia redio ya taifa?

Jibu: Kupitia wimbo wake Republique Du Zaire, ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza kuwa jina la Jamhuri ya Congo litabadilika na kuwa Zaire.

Mshindi: Arthur Chunguli kutoka Maragoli, Kenya
Moses kutoka Dar es Salaam
Salim Hassan Zani kutoka Msambweni, Kenya

Shangazi wa Franco, Elizabeth Masaka, akiwa nyumbani kwao Sona Bata - magharibi mwa Congo, mahali alikozaliwa mwanamuziki huyo.





Siku ya tano: Oktoba 09

Swali: Tupe jina la msanii ambaye hakuwepo kwenye bendi ya TP OK Jazz, lakini alikuwa mshindani mkubwa wa Franco?

Jibu: Pascal Rouchereau aka Tabu Ley

Mshindi: Orest Masue kutoka Norway
Shaibu Semhan kutoka Same, Tanzania
Baluku Kassim kutoka Kampala, Uganda


Picha kumbukumbu ya Franco

Kama sehemu ya vipindi maalum, waandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Noel Mwakugu na Lubunga Bya’ombe, walikuletea mfululizo wa taarifa za kina, wakichambua maswala mbali mbali kama vile mwanzo wa Franco na kipaji chake cha muziki, ushahiwishi wake katika muziki wa Kongo na mitizamo yake ya kisiasa pamoja maisha ya familia yake.




Emongo Luambo akiwa Club Un Deux Trois, iliyomilikiwa na Franco na makao makuu ya TPOK Jazz, mashabiki wa rhumba walithamini club hicho kama hekalu la Rhumba. Sasa hivi Emongo ndiye anayemiliki club hiyo ila siyo maarufu kama ilivyokuwa zamani.




Sheria na kanuni za kushiriki shindano kuhusu maisha na muziki Franco Luambo Makiadi

1. Tuma majibu ya swali pamoja na anwani yako ukianza na jina FRANCO kwa nambari ya ujumbe mfupi wa simu ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC: + 44 77 86 20 20 05.

2. Majibu yote yatapokewa kuanzia matangazo ya Amka na BBC saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja jioni wakati wa matangazo ya Dira ya Dunia. Shindano litaanza Octoba tarehe tano (5) hadi tarehe tisa (9) mwaka 2009.

3. Ujumbe wowote utakaopokewa bila jina FRANCO likiwa mwanzo hautakubalika kwenye shindano.

4. Majibu yote lazima yawe kwa KISWAHILI.

5. Mshindi atatangazwa kwenye kipindi cha Dira ya Dunia kila jioni na katika matangazo ya Amka na BBC


Lutumba Simaro akiendeleza kazi ya muziki, ni mmoja wa wanamuziki waliokuwa na Franco wakati wa uhai wake.



6. Jina la mshindi lita chapishwa kwenye tovuti hii www.bbcswahili.com

7. Mshindi atapokea zawadi ya CD ya Franco Luambo Makiadi iliyotiwa saini na mototo wake wa kiume Emongo Luambo.

8. Idhaa ya Kiswahili ya BBC itagharamia kutuma zawadi hiyo kwa mshindi au anaweza kuipokea kwenye ofisi zetu nchini Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

9. Uamuzi wa BBC kuhusu matokeo hautabatilishwa.

10. Wafanyakazi wa BBC na jamaa zao hawaruhusiwi kushiriki kwenye shindano.

No comments:

Post a Comment