KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 30, 2009

Klaus aisikiza EU


Rais wa tume ya Ulaya amesema wamefanikiwa kuvuka kizuizi cha mwisho cha kisiasa

Viongozi wa muungano wa EU ambao wamekuwa wakikutana mjini Brussels, wameafikiana kuhusu maneno yatakayotumiwa, katika kuondoa kizingiti ambacho kimekuwa kikizuia makubaliano kamili kuafikiwa ya mkataba wa Lisbon.
Mkataba huo wa Lisbon utarahisisha utaratibu kufanya uamuzi miongoni mwa mataifa 27 ya muungano huo.

Rais wa Czech, Vaclas Klaus alikuwa amekataa kutia saini mkataba huo.

Bwana Klaus alikuwa ameelezea kwamba maelezo kuhusiana na mapendekezo ya haki za kimsingi yangeliwawezesha Wajerumani waliofukuzwa kutoka Czechoslovakia wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia kurudi nchini humo na kudai mali yao.

Viongozi wa EU wamekubaliana nchi ya Czech ina uhuru wa kutozingatia sehemu hiyo ya mkataba.

No comments:

Post a Comment