KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, October 26, 2009
JK KATIKA NJIA YA MSAADA.
KWA KWELI MAISHANI, TUNAJIFUNZA MAMBO MENGI. UKIANGALIA MAISHA YA VIONGOZI HUWA NIYENYE MAJUKUMU MAKUBWA NA YENYE KUHITAJI UANGALIFU NA VIPIMO VYA HALI YA JUU.
KUNA WATU AMBAO WANAZALIWA NA KUFA, HAWAJAWAHI HATA KUONA VIONGOZI WAO KWA MACHO, LAKINI KWA KARNE YA SASA TUNA VYOMBO VINGI (RUNINGA, COMPUTER AU SIMU), VYE NYE UWEZO WA KUTUONESHA, SURA, UTENDAJI, BIDII…….N.K YA VIONGOZI WETU.
KWA MFANO WA RAIS WETU WA SASA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, NI RAIS MWENYE TASWIRA YA KUPENDEZA KWA KUMUANGALIA, VITENDO, JITIHADA……NK, KATIKA UTEKELEZAJI.
HAKUNA UONGOZI WENYE KUKOSA UPINZANI WA MANENO NA VITENDO KWA SABABU HUWEZI KUWARIDHISHA BINAADAMU WOTE. NA NDIO MAANA BAADHI YA BINAADAMU WALIAMUA KUWAUWA MANABII (YOHANA, SAMSONI, ZAKARIA,…….N.K)WA MUNGU, KWASABABU YA KUOGOPA KUTEKELEZA HAKI.
DR. JK LICHA YA KUKUTANA NA MITIHANI KAMA, UFISADI, TATIZO LA UMEME, NJAA, UJAMBANZI, UMASIKINI WA WATANZANIA, UPUNGUFU WA ELIMU, ZAHANATI, MIUNDO MBINU YA NCHI, MARANYINGINE HUJIKUTA (DR. JK), AKISAIDIA WATU KATIKA NJIA ZA AINA NYINGI KWAMFANO WA PICHA ILIOKO HAPO KWENYE PAGE, INAONESHA RAIS AKIMSAADIA DADA FULANI KUBEBA NDOO YA MAJI. HATUWEZI KUSEMA KWAMBA TABIA HII KWA DR. JK NI NGENI. LA , BALI DR. JK ALIJALIWA MOYO WA KUISHI KATIKA MAZINGIRA YA USHIRIKIANO NA UPENDO KATIKA MAPITO YAKE.
TANZANIA NI MFANO WA VIONGOZI WENYE KUSHIKA NYADHIFA MBALI MBALI NA ZENYE UMUHIMU NA MASLAHII NDANI YA NCHI NA NJE YA NCHI. KWA MFANO MOTO WA KENYA ULIZIMWA KWA USHIRIKIANO WA VIONGOZI( RAIS JK NA RAIS MTAAFU BENJAMIN W. MKAPA) WA TANZANIA.
NI NCHI NGAPI ZA AFRIKA AMBAZO HAZIWEZI KUSAHAU MSAADA WA TANZANIA JUU YAO. KUNA BAADHI YA NCHI AMBAZO HAZIWEZI KUSAHAU JAMBO HILO NAZO NI :
ANGOLA, MSUMBIJI, ZIMBABWE, SOUTH AFRICA, CONGO, RWANDA, BURUNDI, COMORO……..N.K.
TANZANIA NI NCHI YENYE HIFADHI NZURI YA AMANI, UTULIVU NA UPENDO.
UKITAKA KUJUA KUHUSU AMANI YA TANZANIA, UTAANGALIA MFUMO WA MAKABILA. TANZANIA INA MAKABILA MENGI, LAKINI YOTE YANATUMIA LUGHA MOJA KAMA ISHARA YA MAWASILIANO NA ALAMA YA UPENDO.
DR. JK AMEPATA VYEEO VIKUBWA NDANI NA NJE YA NCHI YAKE. VYEO HIVYO NI VIKUBWA NA VYENYE KUHITAJI MTU MWENYE AKILI TIMAMU NA UWEZO WA KIROHO NA MWILI. NIJAMBO LA TANZANIA KUJIVUNIA KUWA NA RAIS AMBAO WAMEMUAMINI NA AKAAMINIWA NA AFRIKA NZIMA KWA KUMFANYA MWENYEKITI( NI KAMA RAIS WA AFRIKA) WAKE. DR. JK ALIANZA KAZI YAKE YA KUONGOZA NCHI ZOTE ZA AFRIKA NA AKAIMALIZA SALAMA NA HII NI HATUWA YENYE KUMB KUMBU JUU YA AFRIKA HASA TANZANIA. HILI NIJAMBO LA KUMPONGEZA DR. JK KWA JITIHADA YAKE, NA KUMUOMBEA MUNGU KUMZIDISHIA ULINZI JUU YA NAFSI YAKE NA KUMTENGEZEZEA MAZINGIRA YA KUPAMBANA NA UFISADI, NJAA, UJAMBAZI, UMEME, UMASIKINI………N.K.
KATIKA ELIMU DR. JK AMEJITAHIDI KUPANDISHA KIWANGO CHA ELIMU, KUTOKA KATIKA KUNDI LA WANAFUNZI 42,000 WANAOJIUNGA NA VYUO VIKUU NA KUFIKIA HATUA YA WANAFUNZI 92,000
( DR. JK ALIONGEZA 50,000 KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 3.5).
HII NI HATUWA YENYE MSINGI WA MAENDELEO YA NCHI KWA WATU WENYE UWEZO WA KUPENDA MAENDELEO YA NCHI ZAO NA NIVYEMA KUSHUKURU NA KUSAIDIA KILA HATUA NJEMA, BADALA YA KUPINGA KILA JAMBO KATIKA MSINGI WENYE UPUNGUFU WA UCHAMBUZI. UPINZANI MZURI UNAFANYWA KATIKA KUENDELEZA MAZURI NA KUONDOA TAFAUTI ZA NAFSI KATIKA MSINGI WA VIPIMO VYA HAKI. KUNA TAFAUTI YA KUPENDA TIMU NA MCHEZO. KWA MTU MWENYE KUPENDA TIMU, HUONA TIMU NYINGINE HAZIFAI, LAKINI KWA MTU MWENYE KUPENDA MCHEZO, HUWA NI MTU MWENYE KUPENDA KILA MCHEZO WENYE KUVUTIA. UKIPENDA MCHEZO UTAKUWA NA TIMU NYINGI NA UNAKUWA NA UWEZO MKUBWA WA KUFAHAMU MCHEZO, LAKINI UKIWA NA TIMU, HATAKAMA TIMU NYINGINE ZITACHEZA VIZURI, UTAONA KWAMBA HAWANA LOLOTE.
KWA NINI ?
KWA SABABU, UNACHOKIPENDA NI TIMU, SIO MCHEZO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment