KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 30, 2009

FURAHA ni msingi wa maisha bora




FURAHA NI KIFAA KINACHOTOA UTULIVU NDANI YA NAFSI AU BINAADAMU.MSINGI WA FURAHANI NI UTULIVU WA MWILI NA ROHO.UTULIVU WA MWILI NA ROHO UNATENGENEZA MATUMAINI NA UPENDO NDANI YA NAFSI.
NAFSI NI MUUNGANO WA MWILI NA ROHO. ROHO NI KIUNGO KINACHOONGOZA MWILI WA BINAADAMU KATIKA MANENO,HISIA NA VITENDO. MWILI NI KIFAA KINACHOMWEZESHA BINAADAMU KUONA,KUTEMBEA,KULA,KUNUSA,KUPUMUA,…...N.K

MSINGI WA FURAHA NI UPENDO AU MAPENZI YA MTU AU WATU JUU YA BINAADAMU AU VIUMBE WENGINE. UPENDO UNA MISINGI MIWILI MIKUBWA NAYO NI :

• MANENO


• VITENDO

MANENO : MANENO NI UMBILE LA HISIA ZA MOYO JUU YA JAMBO FULANI. BINAADAMU ANAWEZA KUPENDA AU KUCHUKIA KUPITIA HISIA ZAKE ,JUU YA MANENO FULANI.

MANENO YA NATOA MSIMAMO WA NAFSI JUU YA KITU AU JAMBO FULANI. BINAADAMU ANAWEZA KUJUA KWAMBA ANAPENDWA AU ANACHUKIWA KUPITIA MANENO YA UPANDE WA PILI.
MANENO HUWA NI SILAHA AU HUDUMA YA KWAZA YA NAFSI. MANENO YANAWEZA KUONDOA HESHIMA,UAMINIFU,FURAHA,…...JUU YA NAFSI FULANI KUTOKANA NA MUUNDO AU TAFSILI YAKE KATIKA MAZUNGUMZO AU MAHALA HUSIKA.

VILE VILE MANENO YANAWEZA KUJENGA UAMINIFU,FURAHA,UPENDO,MATUMAINI,UTULIVU……..N.K.

VITENDO : VITENDO AU MATENDO NDIO MSINGI WA UTENDAJI WA NAFSI HUSIKA. NAFSI ILI IDHIHIRISHE UKWELI WA MANENO YAKE, INAHITAJI KUTUMIA SILAHA AU KIFAA CHA MATENDO ILI IWEKE SAWA JAMBO HUSIKA.

MATENDO YA NAFSI YANAWEZA KUJENGA AU KUVUNJA FURAHA NA UTULIVU WA SEHEMU HUSIKA. KILA NAFSI INAKUWA NA MTAZAMO AU MAONI JUU YA MATENDO AU KITENDO FULANI, KUTOKANA NA VIGEZO VYAKE VYA ELIMU JUU YA JAMBO HUSIKA. MATENDO MAZURI YANAJENGA MAMBO MAZURI NA KUIMARISHA MLANGO WAKE WA FURAHA NA AMANI NA UTULIVU.

UDHAIFU WA MANENO NDIO UDHAIFU WA MATENDO NA UIMARA WA NAFSI UNATOKANA NA ELIMU YA KUTOSHA ( KUJUA FAIDA,HASARA,UMUHIMU,MADHARA...N.K ) JUU YA MANENO NA VITENDO VYAKE. UJUZI WA MATUMIZI YA MANENO NA VITENDO NI KINGA YA NAFSI NYINGI KATIKA ENEO HUSIKA. HEKIMA YA MTU INATOKANA NA UKWELI KATIKA MAAMUZI YA MANENO YAKE NA MATENDO YAKE. KULIKO MANENO NA MATENDO MAZURI HUONGOZWA NA FURAHA.

1 comment: