KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 20, 2009

China yaahidi kuikomboa meli iliyotekwa


China imeahidi kufanya kila liwezekanalo kuikoa meli ya mizogo ikiwa na mabaharia 25 iliyotekwa na maharamia katika Bahari ya Hindi.

Meli hiyo iitwayo De Xin Hai ilitekwa mapema siku ya Jumatatu ikiwa kiasi cha kilometa 1,100 mashariki mwa pwani ya Somalia.

Meli hiyo iitwayo De Xin Hai ilitekwa mapema siku ya Jumatatu ikiwa kiasi cha kilometa 1,100 mashariki mwa pwani ya Somalia.


Kwa upande mwengine maharamia hao wameonya jaribio lolote la kuiokoa meli hiyo, litahatarisha maisha ya mabaharia.

Umoja wa Ulaya wenye manowari zake za kijeshi zinazopambana na uharamia baharini, umesema meli hiyo inafuatiliwa kwa karibu na inavyoonekana mabaharia wapo katika hali nzuri.
Utekaji huo unaonekana ni wa kwanza kufanyika eneo baina ya Seychelles na Maldives, hali inayoonesha maharamia wamejitanua katika harakati zao.



De Xin Hai, inamilikiwa na kampuni ya meli ya Qingdao Ocean Shipping, ilikuwa ikisafirisha makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini kuelekea India.

No comments:

Post a Comment