KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, June 1, 2009
Sri Lanka imekataa kuruhusu mashirika ya kimataifa kufanya uchunguzi, au kuwashtaki wanajeshi wa nchi hiyo, kwa tuhuma za uki-ukaji wa haki za kibinaa
Sri Lanka imekataa kuruhusu mashirika ya kimataifa kufanya uchunguzi, au kuwashtaki wanajeshi wa nchi hiyo, kwa tuhuma za uki-ukaji wa haki za kibinaadamu, katika vita na wapiganaji wa Tamil Tigers.
Waziri wa mashauri ya Nchi za Nje, Rohitha Bogollagama, alisema mahakama ya Sri Lanka, yana uwezo wa kushughulika na swala hilo.
Waziri huyo amesema kuwa Sri Lanka, ni nchi huru yenye mfumo wake wa sheria, na mahakama yake huru yatafanya uchunguzi kama kuna malalamiko yoyyote.
Bwana Rohitha Bogollagama, alizitoa maanani, shutuma kwamba mauaji ya kikabila yalitokea siku za mwisho za mapambano na wapiganaji wa kiTamil.
Ameelezea tuhuma za makundi ya kupigania haki za kibinaadamu kuwa ni uzushi, uliokusudiwa kulipa sifa mbaya jeshi la Sri lanka.
Mashirika ya haki za kibinaadamu, na maafisa wa Umoja wa Mataifa, wametoa wito kufanywe uchunguzi, kuhusu mauaji ya maelfu ya raia, katika mapambano hayo.
Serikali ya Sri Lanka, ilitangaza wiki mbili zilizopita, kuwa imewashinda wapiganaji; na Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje, amesema anataraji kuwa kumalizika kwa vita, kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa asili-mia-tatu kila mwaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment