KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, June 3, 2009
Al-Qaeda yawaonya waislamu dhidi ya kumshabikia Obama
Huku Rais wa Marekani Barack Obama akianza ziara yake mashariki ya kati, kundi la Al-Qaeda limewaonya waislamu dhidi ya kumshabikia.
Naibu kiongozi wa kundi hilo Ayman al Zawahiri amemwita rais Obama kama mhalifu.
Al-Qaeda yawaonya waislamu
Huku Rais wa Marekani Barack Obama akianza ziara yake mashariki ya kati, kundi la Al-Qaeda limewaonya waislamu dhidi ya kumshabikia.
Naibu kiongozi wa kundi hilo Ayman al Zawahiri amemwita rais Obama kama mhalifu.
Bwana Zawahiri alitoa kauli hiyo siku moja kabla rais Obama kufanya mazungumzo na Mfalme Abdullah nchini Saudi Arabia.
Hapo alhamisi rais huyo wa Marekani atahutubu katika chuo kikuu mjini Cairo.
Ayman Al Zawahiri ndiye mwasisi wa kundi la Islamic Jihad lililoko nchini Misri na inadaiwa kuwa ni mkuruba wa kiongozi wa Al Qaeda Osama bin Laden.
Kauli ya bwana Zawahiri ilichapishwa kwenye tovuti yenye uhusiano na kundi la Al Qaeda
Katika waraka wake ambao unachukuliwa kama tisho dhidi ya rais wa marekani, Zawahiri anamtaja rais obama kama muhalifu na anawasihi wailsamu wapuuze ujumbe wake wa kutaka kuleta maridhiano kati ya marekani na waislamu kote duniani.
Badala yake, kiongozi huyo wa Al Qaeda anawasihi waislamu wazingatie maovu na maafa yanayotekelezwa dhidi ya kundi la taleban katika bonde la SWAT na wanajeshi wa pakistan, mshirika wa karibu wa marekani.
Hapo kesho, Rais Obama anatarajiwa nchini Misri ambapo atatoa hotuba katika chuo kikuu cha cairo. Hotuba hiyo imelenga kuashiria mwanzo mpya wa uhusiano mzuri kati ya marekani na nchi za kiarabu.
Rais Obama atatoa hotuba hiyo chini ya ulinzi mkali na baadhi ya watakaohudhuria mhadhara huo ni viongozi wa ngazi za juu wa kundi linaloegemea itikadi kali za dini la muslim brotherhood.
Viongozi hao wameupokea vema zaira ya rais Obama lakini wamesisitiza kuwa lazima achukue msimamo thabiti kuhusu mzozo kati ya Israel na palestina na afanye kila juhudi kuimarisha uhusiano kati ya marekani na waislamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment