KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 26, 2009

Misitu yaangamia kwa kasi kubwa Afrika

Misitu yaangamia kwa kasi kubwa Afrika

Ripoti iliyotolewa inaonesha misitu barani Afrika inatoweka kwa kasi kuliko ilivyo sehemu nyingine za dunia kutokana na kukosekana kutokuwepo umiliki wa aradhi unaotambulika.

Ripoti iliyotolewa inaeleza misitu ya Afrika inaangamia kwa kasi kubwa tofauti na maeneo mengine duniani kutokana na kukosekana mikakati ya kumiliki ardhi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Haki na Mali chini ya asilimia mbili ya misitu ya Afrika ipo chini ya umiliki wa jamii, ikilinganishwa na nchi za Amerika Kusini na Asia.

Kiwango cha ukataji miti Afrika ni kikubwa mara nne zaidi ya wastani wa ukataji isitu katika sehemu nyingine za duniani.

Kwa kiwango cha sasa, itachukua miaka 260 kwa nchi za Bonde la mto Congo kufikia hatua ya mageuzi iliyopatikana katika misitu ya Amazon.

Hatua ya kumilikisha ardhi inaweza kusidia kuinusuru misitu, kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa na pia itasaidia kuondoa umasikini, kwa mujibu wa ripoti iliyopewa jina Ukaguzi wa Umilikaji wa Misitu ya nchi za Joto, Hali ilivyo, Changamoto na mikakati.

Taarifa ya uchunguzi huo ilitolewa mjini Yaunde Cameroon, katika mkutano wa wawakilishi wa jamii zinazoishi katika maeneo ya misitu katika Afrika, Amerika Kusini na Asia.

No comments:

Post a Comment