KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 26, 2009

Mdororo wa Uchumi waivaa Afrika kusini



Waziri Trevor Manuel wa Afrika kusini
Uchumi wa Afrika kusini umekumbwa na mdororo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992, kufuatia kupungua kwa kasi ya uzalishaji viwandani halikadhalika sekta ya madini.
Uchumi wa nchi yenye Uchumi bora barani Africa imerekodi upungufu wa kiwango cha hadi asili mia 6.4% kati ya mwezi Januari na March, ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka jana.

Hiki ndio kiwango kikubwa cha upungufu tangu mwaka 1984 kikifuatiwa na mdororo wa asili mia 1.8% kila mwaka katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Sekta ya ujenzi hata hivyo imeimarika kutokana na mashindano ya mpira ya Kombe la Dunia yanayopangwa kufanyika huko.

Afrika kusini imenufaika chini ya mpango kabambe wa serikali wa uwekezaji katika mipango ya mashindano ya mpira ya mwaka 2010.

Takwimu zilizofanywa na kampuni huru 'Statistics South Africa, imebaini kupungua kwa uzalishaji viwandani pamoja na uwindaji wanyama pori vimechangia mno mdororo huo.

Makampuni ya kuchimba migodi yameathiriwa na mdororo wa uchumi duniani

No comments:

Post a Comment