KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, March 19, 2009

CHETI CHA KUJENGA FAMILIA HALALI

UMOJA WA FAMILIA NI PUNGUZO LA WATOTO WA MTAANI , NA NI KITEGA UCHUMI CHA AMANI NA UTULIVU KATIKA JAMII.


UMMOJA NI NGUVU, MOJA INAYO JIUNGA NA NGUVU YA PILI AU ZAIDI KWA LENGO LA KUIMARISHA UIMARA WA KILA MWANACHAMA WA MUNGANO.

MUNGANO UNATOKANA NA KIUNGANISHI MAALUMU. KIUNGANISHI CHA MUNGANO KINAWEZA KUWA NI NDOA,NGUVU ZA KIJESHI, WAKULIMA,WALIMU,WAVUVI……..Etec.

UKIJA KWA UPANDE WA NDOA UTAKUTA KUNA MUUNGANO WA HALI YA JUU. UKUBWA WA NDOA KAMA KIUNGANISHI CHA FAMILIA NIKAMA SILAHA YA NYUKRIA INAVYOANGAMIZA WATU NA VITU. KIUNGANISHI CHA KOO MBILI KATIKA JAMII NI NDOA. NDOA INA UWEZO WA KUUNGANISHA VITU NA NYOYO ZA BINAADAMU. NDOA INAWEZA KUUNGANISHA MTU MWEUPE NA MWEUSI,MREFU NA MFUPI,TAJIRI NA MASIKINI,KILEMA NA MTU MZIMA…….Etec.

NDOA INA TOA HESHIMA JUU YA MSIMAMIZI WA UKOO NA WANACHAMA WA UKOO. HESHIMA HII INATOKANA NA MALEZI BORA WALIOMPA MTOTO WAO AKAWEZA KUKUA NA KUJIZUILIA KUISHI NA MWANAMUME BILA IDHINI YA UKOO WAKE. MTOTO ANAPOISHI NA MWANAMUME AU MWANAMKE BILA IDHINI YA WAZAZI WAKE, TAYARI AMEKENGEUKA MILA NA DESTURI NA HESHIMA NA TAHADHIMA YA UKOO HUSIKA.HAKUNA MZAZI ANAEFURAHI ANAPOONA MTOTO WAKE AKIMKOSEA ADABU NA KUMDHARAU AU KUWADHARAU WATU WENGINE. NA HAKUNA MZAZI ANAEFURAHI ANAPOSIKIA MTOTO WAKE AKIZINI AU AKIZINIWA NA MTU BILA IDHINI YA NDOA. JAMBO HILI WAZAZI WOTE HAWAALIKUBALI NA MTU ANAPOJARIBU KUFANYA HAYA HUITWA MBAKAJI. MBAKAJI NI YULE AMBAYE AMEWEZA KUZINI NA MTU KWA NGUVU,BILA IDHINI YAKE. LAKINI UNAPOKUJA KWA UPANDE WA PILI MBAKAJI ANAWEZA KUA KILA MTU ANAEZINI NA MTOTO WA MWENZIE BILA IDHINI YA WAZAZI HUSIKA. LICHA YA MUNGU KUKATAZA ZINAA VIUMBE WAKE , NA HAKUNA MZAZI ANAE FURAHI ANAPOSIKIA KWAMBA MWANAE HUBADILISHA WANAUME KILA KUKICHA.ZINAA INACHAFUA FAMILIA NA ATHARI HIZO HUATHIRI HADI UKOO HUSIKA. MKOSAJI UMOJA KATIKA FAMILIA NI DOSARI KUBWA KATIKA FAMILIA NA UKOO HUSIKA. LICHA YA WATU WENGI KUHOFIA AU KUJITAHIDI KULINDA WATOTO WAO NA KITENDO CHA ZINAA, MARANYINGINE HUJIKUTA KATIKA MASHAMBULIZI YA KIZAZI AU WATOTO WAO JUU YA UHURU WAO ( UHURU WA MTOTO KUISHI AU KUJITEGEMEA NA AKIISHI ANAVYOTAKA BILA KUONGOZWA NA WAZAZI AU KUPINGA MCHANGO WA WAZAZI JUU YA MAAMUZI FULANI ).WAZAZI WAKIAMINI KWAMBA WAO NDIO WAFUNZAJI BORA WA WATOTO WAO, BILA KUJALI MCHANGO WA WANACHAMA WA FAMILIA,JAMBO HILI LINAWEZA KULETA UTATA KATIKA FAMILIA HUSIKA NA ATHARI ZIKASAMBAA KATIKA UKOO MZIMA NA JAMII PIA.

IKIWA KATIKA NDOA, FAMILIA MBILI HUUNGANA NA KUTENGENEZA MUUNGANO WA KOO MBILI,KISHA FURAHA ,AMANI NA UTULIVU UKATAWALA KATIKA NYOYO ZA WASHIRIKI WOTE,KWANINI IKIWA MZAZI WA KIKE AKIJIFUNGUA MTOTO ANAWAITA AU WANAITA AU WANAWAPA TAARIFA, WANACHAMA WOTE WA KOO ZOTE MBILI ( UPANDE WA MKE NA UPANDE WA MME ). NA KUFURAHIA KUZALIWA KWA MTOTO HUSIKA,NA ANAPOPEWA JINA WATU WOTE WANAFURAHIA KUZALIWA KWA MTOTO NA KUPEWA JINA ZURI LA UKOO WA BABA ). KINACHOSHANGAZA NI PALE AMBAPO MTOTO ANAPOCHUKUA HATUWA ZA KUJITEGEMEA, KITENDO HICHO HUONEKANA KWAMBA NI MZIGO WA WAZAZI WA MTOTO HUSIKA SIO WA MUNGANO WAKOO. NA MARA NYINGINE WAZAZI WANAPOKOSEA KATIKA MALEZI HUJIKUTA KATIKA MIGOGORO BAINA YAO NA WATOTO WAO.KITENDO HICHO HULETA PICHA MBAYA BAINA YA FAMILIA HUSIKA NA KOO HUSIKA NA KWA JAMII PIA. KUSHINDWA KWA WAZAZI KUONGOZA WA TOTO WAO KITABIA, NDICHO CHANZO CHA NGONO ZEMBE NA
MALALAMIKO YASIYOISHA JUU YA FAMILIA NA UPUNGUFU WA UPENDO JUU YA KOO HUSIKA.IKIWA NDOA NI KINGA YA ZINAA , NINI KIFANYIKE ILI IDUMU?

No comments:

Post a Comment