KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, May 12, 2012

Wanachama 136 wajiengua CUF

Mzimu wa kufukuzwa uanachama kwa Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, na wenzake 10, umezidi kukiandama Chama cha Wananchi (CUF), baada ya wanachama wake 136, mkoani Tanga, akiwamo aliyegombea ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 na 2010, Mohammed Salim Siu, kujitoa katika chama hicho. Habari zilizolifikia NIPASHE jijini Dar es Salaam kutoka Tanga zinaeleza kuwa Siu na wenzake walifikia uamuzi huo baada ya kurejesha kadi za CUF katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika jengo la Makorora Community Centre, mjini humo jana. Uamuzi huo ulifikiwa na Siu na wenzake kwa sababu mbalimbali, ikiwamo kile walichodai kuwa ni kuchoshwa na migogoro ndani ya chama isiyokuwa na ufumbuzi wa busara kiasi cha kusababisha wanachama kukikimbia chama kutokana na maamuzi yasiyoheshimu mawazo ya wanachama.

No comments:

Post a Comment