KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, February 28, 2011

Waislam Ujerumani wamkosoa waziri mpya wa ndani




Mashirika na jumuiya za Kiislam nchini Ujerumani zimeyakosoa matamshi yaliyotolewa na Waziri mpya wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Hans-Peter Friedrich.

Waziri huyo mpya wa ndani alilielezea kongamano la Kiislam linalowajumuisha pamoja wanasiasa na wawakilishi wa jumuiya ya Kiislam yenye waumini kiasi ya millioni nne hapa Ujerumani, kwamba kongamano hilo ni kama tukio la kujifaharisha tu.

Katika hotuba yake ya kwanza tokea kuteuliwa kushika wadhifa, huo Bwana Friedrich alisema kuwa hakuna uthibitisho wowote kama Uislam kihistoria ulikuwa ni sehemu katika jamii ya Ujerumani.

Matamshi hayo yamepingana na yale yaliyotolewa na Rais wa Ujerumani Christian Wulff



Mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina kuanzishwa rasmi leo Washington




Viongozi wa Israel na Palestina wanaanzisha rasmi mazungumzo ya amani hii leo. Kundi la Hamas linapinga vikali matokeo ya mkutano wa Annapolis

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, amesema viongozi wa Israel na Palestina leo wataanzisha rasmi mazungumzo ya amani katika ikulu ya Marekani mjini Washington.



Kuanzishwa kwa mazungumzo hayo kunafanyika baada ya mkutano wa kihistoria kuhusu amani ya Mashariki ya Kati kufanyika mjini Annapolis katika jimbo la Maryland.



Katika mkutano huo viongozi wamekubaliana kwamba taifa huru la Palestina litaundwa kufikia mwishoni mwa mwaka ujao 2008.



Condoleezza Rice amesisitiza maneno yaliyosemwa na rais George W Bush kwamba maswala yote ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi yatatuliwa.



Rais Bush amesema huu ni wakati muafaka kuwadhihirishia Wapalestina kwamba ndoto yao ya kuwa na taifa huru inaweza kufikiwa katika meza ya amani. Aidha kiongozi huyo amesema kwa wakati huu machafuko yanayohubiriwa na wanamgambo wenye itikadi kali ni kikwazo kikubwa kinachozuia kuundwa kwa taifa huru la Palestina.



Rais Bush binafsi amesema amejitolea kwa dhati kutumia muda wake uliosalia kama rais wa Marekani kutafuta suluhisho la mataifa mawili la mgogoro wa Mashariki ya Kati.



Wakati haya yakiarifiwa maelfu ya wafuasi wa kundi la Hamas katika eneo la Ukanda wa Gaza wamefanya maandamano makubwa katika barabara za mjini Gaza kuyapinga matokeo ya mkutano wa Annapolis nchini Marekani.



Kiongozi wa Hamas, Ismail Haniya, amesema makubaliano yoyote yatakayofanywa na rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, Mahmoud Abbas, hayatakubalika.



Haniya, ambaye alitimuliwa na rais Abbas kutoka kwa wadhifa wake wa uwaziri mkuu, amekataa kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Wapalestina na Israel.



Muandamanaji mmoja ameuwawa mjini Hebron huko Ukingo wa magharibi wa mto Jordan wakati machafuko yalipozuka kati ya maafisa wa usalama walio watiifu kwa rais Mamhoud Abbas na wanamgambo wanaomuita msaliti




Rais Abbas kuugomea mpango wa amani wa Israel


Rais Mahmmoud Abbas wa Mamlaka ya Palestina amesema hatakubaliana na hatua zozote za amani za Israel iwapo hatua hizo zitaambatana na mipaka ya muda kwa ajili ya taifa jipya la Palestina.




Rais Abbas akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hii leo mjini Ramallah,amesema bado hajafahamishwa juu ya mpango huo mpya wa amani ambao Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netenyahu anatarajiwa kuutangaza katika wiki zijazo.

Matamshi hayo ya Rais Abbas yanaashiria tafuti kubwa iliyoko kati ya maafisa wa Israel na Palestina, kuhusiana na suala la mada ipi ya kuanzia katika mazungumzo hayo ya amani yatakayopelekea kuanzishwa kwa taifa la Palestina.




Majeshi ya serikali yatwaa mji Somalia




Majeshi ya Serikali ya mpito nchini Somali yakishirikiana na wanamgambo wanaowaunga mkono, yamefanikiwa kuutwaa mji wa Beledhawo kutoka katika udhibiti wa wapiganaji wa al Shabaab, baada ya mapigano makali yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 15.

Mji huo ambao unapakana na mji wa Kenya wa Mandera na pia mpaka wa Ethiopea, umekuwa kitovu cha harakati za majeshi ya serikali kuwafurusha wapiganaji wa al- Shabaab katika maeneo wanayoyadhibiti.

Kamanda wa majeshi hayo ya serikali Kanali Mohamud Ali Shire amethibitisha taarifa hizo za kuutwaa mji huo wa Beledhawo na kusema kuwa wameuawa zaidi ya wapiganaji 20 wa al-Shabaab.Amesisitiza kuwa wataendelea na harakati zao mpaka kuhakikisha kuwa wamewafurusha kutoka katika maeneo yote ya Somalia waasi hao wa al-Shabaab.






Saudi Arabia yapiga marufuku maandamano


Saudi Arabia imepiga marufuku maandamano yoyote nchini humo.Hatua hiyo imetangazwa na wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo, baada ya jamii ya wachache ya Waislamu wa madhehebu ya Washia kufanya maandamano ya upinzani kwenye jimbo la mashariki ambako kuna uzalishaji mkubwa wa mafuta.


Wizara hiyo ya ndani imeonya kuwa majeshi ya usalama yatatumia hatua zozote kuzuia jaribio lolote la kutaka kukiuka amri hiyo.



Jamii ya Washia ambao ni wachache nchini Saudi Arabia, idadi kubwa wanaishi katika eneo hilo la mashariki linalopakana na Bahrain ambayo imeshuhudia maandamano ya upinzani yanayofanywa na jamii ya Washia waliyo wengi, dhidi ya utawala wa Waislamu wa madhehebu ya Wasunni.








Wapinzani wa Libya


Wapinzani nchini Libya wamezuia jaribio la majeshi ya serikali ya kuuchukua tena mji wa Zawiya, kilomita 50 magharibi mwa mji wa Tripoli.

Kufuatia mapigano makali siku ya Jumamosi asubuhi, majeshi ya serikali yalilazimishwa kusogea nje ya mji, ingawa baadhi ya taarifa zinasema wamejipanga upya na huenda wakawa wanapanga mashambulizi mapya.

Idadi ya vifo haiko wazi.

Wakti huohuo, wapinzani wanaompinga Kanali Muammar Gaddafi wamechukua udhibiti wa mji wa bandari wa Lanuf, mashariki mwa Tripoli.

Waangalizi wanasema kwa ujumla ni vigumu kujua nani anadhibiti wapi, wakati mvutano wa kuitawala Libya ukiendelea.

Mjini Tripoli, kuna hali ya kujiamini miongoni mwa wanaoutii utawala, huku udhibiti ukionekana kuongezeka mjini Tripoli na maeneo mengine ya kati, kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo huko.

Lakini katika maeneo mengine, waandishi wa habari wanasema waandamanaji wana ari kubwa ya kuuondoa utawala wa Kanali Gaddafi.

Taarifa kutoka Zawiya zinasema mji huo umeshambuliwa kutoka upande wa mashariki na magharibi kutoka kwa wanajeshi wa serikali wenye silaha nzito.




Rais wa Tunisia atoa wito wa uchaguzi





Maandamano Tunisia


Rais wa mpito wa Tunisa Fouad Mebazaa ametoa maelezo juu ya uchaguzi mpya ulioahidiwa kufanyika baada ya kutolewa kwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali.

Bw Mebazaa alisema kupiga kura kwa wawakilishi wa baraza watakaoandika upya katiba utafanyika Julai 24.

Alisema serikali mpya ya mpito itaongoza nchi hiyo mpaka wakati huo.

Bw Mebazaa alisema ataendelea pia kukaa madarakani, licha ya katiba ya sasa kumpa muda maalum kushikilia ofisi kwa muda wa siku 60.

Katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni, aliahidi kukaa madarakani, " tofauti na ilivyovumishwa, mpaka uchaguzi ufanyike, kwa msaada wa wote."

Ombwe ya uongozi
Shirika la habari la Reuters limesema, baada ya kuchaguliwa, baraza la katiba linaweza kuteua serikali mpya au kuwaomba viongozi wa sasa kuendelea hadi uchaguzi wa Rais na wabunge utakapofanyika.

Tunisia imekuwa ikihangaika kurejesha utulivu tangu maandamano makubwa kufanyika ya kumwondoa Bw Ben Ali Januari 14.

Siku ya Jumapili, waziri mkuu Mohammed Ghannouchi alijiuzulu kutoka serikali hiyo ya mpito. Mawaziri wengine sita wameng'atuka tangu wakati huo.

Mwandishi wa BBC aliyopo Tunis Owen Bennett-Jones amesema ombwe ya uongozi aliyoiacha Bw Ben Ali inazidi kudhihirika.

Alisema, utata wa kisiasa umeibuka kutokana na kipengele cha katiba kinachompa Rais wa muda wakati maalum wa siku 60 tu.

Bw Mebazaa alisema, kwakuwa katiba ya sasa haiaminiki tena, atakaa madarakani hata baada ya muda uliotajwa.

Katika hotuba yake, alisema katiba " haiendani na matakwa ya watu baada ya mapinduzi."

Mwandishi wetu anasema, Rais huyo sasa inabidi asubiri na kuona iwapo mipango yake mipya itachochea kuongezeka kwa maandamano au kuungwa mkono zaidi.

Wiki iliyopita, watu watano waliuawa na polisi wakati wa maandamano ya kuipinga serikali wakitaka mabadiliko zaidi.

Takriban mieizi miwili baada ya Bw Ben Ali kukimbia, waandamanaji bado wameweka kambi karibu na ofisi ya waziri mkuu katikakti mwa mji wa Tunis, wakisema hakuna kilichobadilika.

Lakini waandamanaji wengine kwa sasa wanawasihi Watunisia kuacha maandamano na kurejea kazini



Ana mikakati ya kutoroka kwa kukimbia ndoa



MSICHANA mmoja [jina kapuni] [25] mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam amejikuta akichukia wazazi wake kwa kile anachodai kutafutiwa mchumba na wazazi wake kitendo ambacho hajakifurahia.

Msichana huyo mfanyabiashara wa vipodozi maeneo ya Kariakoo amejikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya wazazi kumtafutia mchumba ambaye wao wanadhani angefaa kuishi nae katika maisha.

Hata hivyo katika taarifa fupi aliyotoa msichana amedai anashinikizwa kuolea na mwanamume huyo ambaye ni raia a nchi jirani kwa kuwa ameoneka kuwa na uwezo wa kifedha na wazazi kuonekana kuridhika nae.

Amedai kuwa iwapo wazazi wake wataendelea kumshinikiza kuolewa na mwanaume huyo itamlazimu atoweke jijini Dar es Salaam kwa muda usiojulikana.

Hata hivyo aliiambia nifahamishe kuwa wka sasa hayuko tayari kuolewa na mwanaume wa aina yoyote hadi atimize malengo yake aliyojiwekea.

Amedai katika wazo lake la haraka haraka ameona kutoroka nje ya mji inaweza ikamsaidi kuepukana na hilo kwa kuwa alikuwa akiheshimu wazazi wake



Kamati yapendekeza Dowans iwashwe



KAMATI ya Nishati na Madini imetaka mitambo ya kuzalisha umeme ya Kampuni ya Dowans iwashwe mara moja ili kupunguza tatizo la mgawo wa umeme. Nchini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba (CCM), alitoa taarifa hiyo kwa wanahabari mara baada ya kutoa pendekezo hilo kati ya 30 ya yaliyotolewa na dkadmati hiyo.

Alisema mapendekezo yaliyotolewa ni yale ya dharura kamati imeamuru kupunguzwe megawati 125 zinazotumika katika migodi 4 ya madini ili umeme huo uelekezwe kwa matumizi ya wananchi awa kawaida.

Pia serikali iongeze nguvu ya kuongeza mafuta katika mitambo ya kuzalisha umeme ya IPTL ili iwe na uwezo wa kuzalisha megawati 90 na si kuzalisha megawati 10 hadi 50 kama hivi sasa.

Wakati hayo yakipendekezwa, nayo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetoa siku 21 kwa pande mbili ambazo ni Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Ltd na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) kupeana nyaraka za madai ya fidia ya shilingi bilioni 94 iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) kwa kampuni hiyo.

Aidha, mahakama hiyo imeamuru pia upande wa wapingaji wa fidia hiyo ambao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nao upewe nyaraka hizo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ombi hilo.

Awali Mahakama ya ICC ilitoa hukumu ya kesi ya Dowans dhidi ya TANESCO, Novemba 15 mwaka jana, ambapo iliitia hatiani TANESCO kwa kosa la kuvunja mkataba na Dowans na ikaiamuru iilipe fidia ya shilingi bilioni 94




Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeezea hofu ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ivory Coast


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeezea hofu ya kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Ivory Coast, na kuamrisha walinda amani wake kutumia njiya zote ili kuwalinda raia.

Hapo Alhamisi wanajeshi watiifu kwa Laurent Gbagbo anayeng'ang'ania madaraka licha ya kushindwa kwenye uchaguzi Mkuu waliwafuatilia risasi wanawake waliokuwa wakiandamana mjini Abdijan kumuunga mkono Alassane Ouattara anayetambuliwa kushinda uchaguzi huo kimataifa.

Takriban wanawake sita waliuawa kwenye tukio hilo.Wakati huo huo mshirika wa karibu wa Bw. Ouattara ameitaka jamii ya kimataifa kuchukulia mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast kwa uzito sambamba na hali ilivyo huko Libya.

Mwakilishi wa Kambi ya Ouattara katika Umoja wa Mataifa Youssoufou Bamba amesema wapinzani wao wanatumia silaha za vita kuwalenga raia wasio na hatia



Mahakama yachunguza 'uhalifu'wa Gaddafi




Brega

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu amesema atamchunguza kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, watoto wake wa kiume na viongozi waandamizi kwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Luis Moreno-Ocampo alisema hakuna mwenye haki ya kuwaua raia.

Maelfu ya watu wanadhaniwa kufariki dunia katika ghasia baada majeshi ya usalama kuwalenga waandamanaji katika vurugu zilizoanza Februari 17.

Kanali Gaddafi aliahidi kuendelea kupambana licha ya kukosa udhibiti wa eneo kubwa la nchi hiyo.

Vyanzo vya habari mjini Brega vilisema, mapema siku ya Jumatano majeshi yake yalishambulia kwa kutumia ndege katika mji huo wenye mafuta.

Mashambulio hayo yalifanyika siku moja baada ya kuwepo mapigano baina ya waasi na majeshi ya serikali katika mji ambapo watu 14 walifariki dunia.

Alisema, " Ofisi ya mwendesha mashtaka aliamua kufanya uchunguzi kwa madai ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyofanywa Libya tangu Februari 15."

" Ujumbe wa waandamanaji waliofanya kwa amani walishambuliwa na majeshi ya usalama.

" Katika wiki zijazo ofisi hii itachunguza ni wepi wanahusika zaidi katika mashambulio mazito zaidi, na kwa uhalifu mbaya zaidi uliofanywa Libya."

Lakini mwendesha mashtaka huyo pia alisema upinzani nao utachunguzwa kama ulifanya uhalifu wowote





Nauli daladala Juu, wanafunzi kulipa 150



NAULI za usafiri wa daladala na mkoani Dar es Salaam imepanda maradufu kutokana na kile kilichodaiwa ni kupanda kwa gharama za undeshaji katika sekta hiyo.
Taarifa hiyo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini [SUMATRA] nauli hiyo itaanza wiki ijayo.

Ongezeko hilo limekuja baada ya mamlaka hiyo kupewa ombi na wamiliki wa mabasi jijini Dar es Salaam kulalamikia ongezeko la gharama za uendeshaji wa usafiri huo.

Hivyo nauli za daladala zinazofanya shughuli zake katika barabara ya lami, zimepandishwa kwa asilimia 17.4 ambapo sasa kila msafiri atalazimika kulipa shilingi 27 kwa kila kilometa badala ya shilingi 22.9 kwa kilomita ya awali.

Hatua hiyo ya kupandisha nauli za daladala mkoani Dar es Salaam imekuja siku chache baada ya SUMATRA kuruhusu kupanda kwa nauli ya mabasi yaendayo mikoani nchini kote








Watu watatu wauawa mlipuko Nigeria


Mlipuko wa bomu umetokea katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, na watu wasiopungua watatu waliuwawa kwa mujibu wa polisi wa nchi hiyo.


Ramani ya Nigeria


Maafisa walisema mlipuko huo ulitokea katika mhadhara wa chama cha Peoples Democratic Party huko Suleja, kilomita 40 kutoka Abuja.

Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwaka ujao.

Katikati mwa nchi hiyo kumeibuka vurugu kati ya makundi ya kikabila, kidini na ya kisiasa.

Msemaji wa polisi Olisola Amore alisema bomu hilo lilirushwa kutoka kwenye gari moja lakini haikufikia katikati mwa maandamano hayo na kuanguka karibu na soko iliyokuwa karibu.

Watu watatu waliuawa papo hapo na wengine 21 walijeruhiwa.

Alisema kuwa hakuna kundi lolote ambalo limejihusisha na shambulio hilo na hakuna aliyekamatwa..

Bw Amore alisema mgombea wa urais wa chama hicho cha PDP, Babangida Aliyi, hakujeruhiwa.

Yushua Shuaib msemaji wa shirika la taifa la utawala wa dharura, NEMA, alisema kuwa shambulio hilo lilitokea baada ya maandamno hayo kumalizika.




Wafiwa Gongolamboto watakiwa kufungua mirathi




NDUGU waliopoteza ndugu zao kutokana na milipuko ya mabomu ya Jeshi la JWTZ Gongolamboto wametakiwa kufungua mirathi Mahakamani ili waweze kupewa rambirambi zao..
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Meck Sadick.

Sadick aliwataka ndugu wa karibu walioteuliwa kusimamia waende Mahakamani kufungua mirathi ili serikali iweze kuwalipa kifuta machozi kilichopangwa wka kila aliyepoteza ndugu katika tukio hilo.

Alisema serikali imepanga kulipa kiasi cha shilingi million 8.5 kwa kila aliyepoteza ndugu kwa ajili ya kuwafuta machozi ndugu hao.

Alisema dhamira ya serikali iliyoazimia ni kukabidhi fedha hizo mapema kwa wanafamilia, ikiwa na kuondoa ubabaishaji katika zoezi hilo



'Nitakufa Hapa Kama Shahidi' - Gaddafi Achachamaa


Kiongozi wa Libya, kanali Muammar Gaddafi amekanusha uvumi kuwa amekimbia nchi na kusema hatakimbia nchi kwasababu ya vurugu zinazoendelea nchini humo na yuko tayari kufa kama shahidi ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
Akiongea kwa hasira huku mara akiipiga ngumi meza kwa hasira, Gaddafi alionya kuwa hataachia madaraka na kuikimbia nchi hiyo kama walivyofanya viongozi wa Tunisia na Misri.

"Mimi ni mpiganaji na mwana mapinduzi toka kwenye mahema ... nitakufa hapa kama shahidi", alisema Gaddafi na kuongeza "Nitapambana mpaka tone la mwisho la damu yangu".

Gaddafi aliwaita waandamanaji wanaomshinikiza ajiuzulu kuwa ni 'Panya' na vijana wanaotumia madawa ya kulevya wanaovishambulia vituo vya polisi.

Gaddafi aliwataka wafuasi wake waingie mitaani kupambana na waandamanji. "Wale wanaompenda Gaddafi ingine mitaani na wala msiwaogope wahuni".






Akiongea toka kwenye mojawapo ya nyumba zake ambayo ilipigwa bomu na Marekani mwaka 1980, Gaddafi mwenye umri wa miaka 68, aliwaonya waandamanaji kuwa wanaovunja sheria za nchi watakumbana na kifo.

Pamoja na jeshi la Libya kutumia nguvu, kuwapiga risasi na hata kutumia ndege za kivita kuwashambulia waandamanji, Gaddafi amedai bado hata hajalipa ruhusa jeshi kuwashambulia waandamanji na atakapotoa ruhusa waandamanaji watajuta.

"Bado sijaruhusu kutumika kwa nguvu kuzuia maandamano, bado sijaruhusu risasi hata moja kufyatuliwa... nitakaporuhusu kila kitu kitaangamia", alionya Gaddafi.

Viongozi wa mataifa mbalimbali wamemuonya Gaddafi kuacha kutumia nguvu kuzuia waandamanaji, jeshi la Libya limelaumiwa kwa kuwaua waandamanaji wengi.

Watu zaidi ya 2,000 wameishauliwa katika mji wa Benghazi pekee ambako maandamano ya kumpinga Gaddafi yalianzia.

Polisi walenga shabaha wamelaumiwa kwa kuwatungua kwa risasi na kuwaua waandamanji wengi wanaompinga Gaddafi.

Pamoja na Gaddafi kutumia nguvu kuzuia waandamanji, maandamano ya kumng'oa yamezidi kupamba moto kutokana na hasira za watu wengi ambao ndugu zao au jamaa zao wameuliwa waziwazi kwa kujitokeza mitaani kumpinga Gaddafi



Kiongozi wa waasi wa Kihutu kushtakiwa Ujerumani





Mahakama ya mjini Stuttgart hapa Ujerumani imemtia hatiani kiongozi wa kundi la waasi wa Kihutu Ignace Murwanashyaka, kwa kuhusika na makosa kadhaa ya uhalifu wa kivita na dhidi ya ubinaadamu.

Ananshutumiwa kwa kuamrisha vitendo vya ubakaji pamoja na mauaji hususan katika makambi ya wakimbizi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa takriban kipindi cha miaka miwili.

Ignace anatuhumiwa kuendesha vitendo hivyo akiwa uhamishoni hapa Ujerumani.Serikali ya Ujerumani ilimkamata Novemba mwaka 2009, na anatarajiwa pia kufunguliwa mashtaka ya kuwa Rais wa kundi la wanamgambo wa Kihutu FDLR tokea mwaka 2001.

Makamu wa rais wa kundi hilo pia anaishi hapa Ujerumani ambapo naye pia atakabiliwa na mashtaka hayo.Kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Mei mwaka huu




Libyan weapons depot blasts kill 19




Miripuko ilioripuka mmoja baada ya mwengine katika ghala la silaha imeuwa watu 19 na kujeruhi wengine madarzeni nje ya mji wa Benghazi unaoshikiliwa na waasi.

Sababu ya miripuko hiyo haikuweza kufahamika mara moja juu ya kwamba wakaazi wengi wa mji huo wamefuta uwezekano kuwa umetokana na mashambulizi ya anga ya vikosi vya kiongozi wa Libya Muoamer Gaddafi.

Waasi wanadhibiti sehemu kubwa ya Libya mashariki na wameufanya mji wa Benghazi kuwa makao makuu yao katika mapambano na vikosi vinavyomuunga mkono Gaddafi.

Wakati huo huo vikosi hivyo vya Gaddafi vimefanikiwa kuingia Zawiyah mji ambao uko karibu na mji mkuu wa Tripoli na ambao kwa siku kadhaa ulikuwa ukipinga utawala wake. Waasi wanasema wameuteka mji wa mwambao wa Ras Lanuf na kuongeza maeneo wanaoyadhibiti mashariki ya nchi hiyo.






'Wanawake Wasioolewa Nitawapa Mume' - Mgombea

Mgombea urais wa nchini Kazakhstan, Amantay Asilbek


Mgombea wa urais nchini Kazakhstan amekuja na kampeni ya urais ya aina yake duniani kwa kutamba kuwa atawapatia waume wanawake wote wa nchini humo ambao hawajaolewa.
Mgombea urais wa nchini Kazakhstan, Amantay Asilbek amewaahidi wanawake nchini humo kuwa atahakikisha wanawake wote ambao hawajaolewa wanapata waume.

"Nchini Kazakhstan kuna wanawake wengi ambao hawajaolewa, hili ni janga la taifa kwani tunawapoteza akina mama wa baadae", alisema Asilbek wakati wa mahojiano na gazeti moja nchini humo.

Asilbek aliendelea kusema kuwa tatizo la wanawake wengi kukosa waume litapatiwa ufumbuzi kwa kuwaruhusu wanaume kuwaoa wanawake zaidi ya mmoja.

Asilbek mwenye umri wa miaka 70 alitamba kuwa hata yeye mwenyewe pia amefikiria kuongeza mke wa pili.

Pamoja na kusapoti wanaume kuoa wanawake wengi, Asilbek alionyesha wazi hataki kumuudhi mwandani wake kwa kumletea mwenzake kwa kusema"
"Wasichana wengi wamekuwa wakija nyumbani kwangu wakiwa na ndoto za kuwa wake zangu, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kuwa na kiwango cha ubora kama cha mke wangu", alitamba Asilbek.

Asilbek alisema kuwa atapigania kuruhusiwa kwa wanaume kuoa wanawake wengi ili kuondoa tatizo la wanawake wengi kubaki majumbani mwa wazazi wao wakiwa wamekosa wanaume wa kuwaoa.

Asilbek, alijaribu kugombea nafasi ya kuwania urais mwaka 1998 lakini aliikosa nafasi hiyo. Alikubaliwa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2005 lakini aliangushwa vibaya.

Safari hii Asilbek amejitosa tena kugombea urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 3 mwezi wa nne mwaka huu.




BAADHI ya wakazi wa Gongolamboto na vitongoji vyake jana walikuwa katika hofu



BAADHI ya wakazi wa Gongolamboto na vitongoji vyake jana walikuwa katika hofu kubwa huku wengine kukimbia na kuacha makazi yao, kutokana na kuona miale ya mwanga inayoruka angani kutoka kwenye kambi ya Jeshi ya Gongolamboto kikosi cha 511 KJ.
Jana kuanzia majira ya saa 4 usiku, miale inayotoa mwanga mkali mithili ya radi ilionekana ikitoka kutoka kwenye kambi hiyo na kuleta hofu kubwa kwa wakazi hao huku wengine kuanza kuchukua watoto wao na kukimbia.

Hivyo kutokana na hofu hiyo baadhi ya wakazi waishio karibu na kambi hiyo walionekana kuhaha kwa hofu na baadhi kuonekana kukimbia na kuacha makazi yao.

Hata hivyo NIFAHAMISHe ilizungumza na mkazi wa karibu na kambi hiyo kwa njia ya simu majira ya saa 4:30 na kubainishiwa hilo.

Majira ya asubuhi baadhi ya wakazi walionekana wakiwa katika msongamano barabarani wakiondoka makazi yao huku wengine wakielekea Uwanja a Taifa



Waziri Mkuu wa Misri Ahmed Shafiq amejiuzulu




Ahmed Shafiq


Baraza la jeshi lilitoa taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyekuwa waziri wa usafiri, Essasm Sharaf, amependekezwa kuunda serikali mpya.

Bw Shafiq aliteuliwa kuwa waziri mkuu siku chache tu kabla ya Rais Hosni Mubarak kujiuzulu tarehe 11 Februari baada ya siku kadhaa za maandamano

Waandamanaji walisema kuwa Bw Shafiq alikuwa mshirika wa karibu sana wa Bw Mubarak.

Baraza kuu la jeshi lilikubali uamuzi wa Bw Shafiq na kumteua Essam Sharaf kuunda serikali mpya lilisema jeshi hilo kupitia ukurasa wao wa face book.

Jumatatu, Misri ilimwekea vikwazo ya kutosafiri Hosni mubarak na familia yake







Miaka miwili jela kwa kuchoma msahafu


MAHAKAMA ya Wilaya ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela pamoja na kulipa fidia ya shilingi 200,000/ Ramadhan Tuma (28) kwa kosa la kuchoma moto kitabu kitakatifu kiitwacho msahafu.
Hukumu hiyo imetolewa mahakamani hapo na Hakimu Khamis Ali Simai baada ya kuridhika na na ushahidi na kupatikana na hatia hiyo.

Hakimu Simai alisema kuwa,upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha makosa hayo dhidi ya mtuhumiwa na atapewa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria kwa kuwa kitendo hicho ni uvunjifu wa amani kwa mujibuwa sheria za Zanzibar.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo mtuhumiwa aliiomba mahakama hiyo impunguziwe adhabu kwa madai kuwa ana familia inayomtegemea akiwemo mke na mtoto pia aliiambia mahakama kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.



Awali ilidaiwa kuwa, Ramadhan Handa Tuma alifanya kosa hilo Novemba 16, mwaka jana, akiwa hadharani kwa makusudi alichoma moto kitabu kitakatifu cha dini ya kiislamu ‘msahafu’ pamoja na juzuu



The Qur’an




The Qur’an (English pronunciation: /kɒˈrɑːn/ kor-AHN; Arabic: القرآن‎ al-qur’ān, IPA: [qurˈʔaːn], literally “the recitation”) is the religious text of Islam,[1] also sometimes transliterated as Quran, Kuran, Koran, Qur’ān, Coran or al-Qur’ān. It is widely regarded as the finest piece of literature in the Arabic language.[2][3][4] Muslims hold that the Qur’an is the verbal divine guidance and moral direction for mankind. Muslims also consider the original Arabic verbal text to be the final revelation of God.[5][6][7][8]

Muslims believe that the Qur’an was repeatedly revealed from Allah to Muhammad verbally through the angel Jibrīl (Gabriel) over a period of approximately twenty-three years, beginning in 610 CE, when he was forty, and concluding in 632 CE, the year of his death.[5][9][10] Followers of Islam further believe that the Qur’an was memorized, recited and written down by Muhammad's companions after every revelation dictated by Muhammad. Most of Muhammad's tens of thousands of companions, called Sahabas, learned the Qur’an by heart, repeatedly recited in front of Muhammad for his approval or the approval of other Sahabas. Muslim tradition agrees that although the Qur’an was authentically memorized completely by tens of thousands verbally, the Qur’an was still established textually into a single book form shortly after Muhammad's death by order of the first Caliph Abu Bakr suggested by his future successor Umar. Hafsa, Muhammad's widow and Umar's daughter, was entrusted with that Quran text after the second Caliph Umar died. When Uthman, the third Caliph, started noticing slight differences in the Arabic dialect; he requested Hafsa to allow him to use the Qur’an text in her possession to be set as the standard dialect, the Quraish dialect aka Fus'ha (Modern Standard Arabic). Before returning that Qur'an text to Hafsa; Uthman immediately made several thousands of copies of Abu Bakar's Qur’anic compilation and ordered all other texts to be burned. This process of formalization of the orally transmitted text to Abu Bakar's Qur'anic text is known as the "Uthmanic recension".[11] The present form of the Qur’an text is accepted by most scholars as the original version compiled by Abu Bakr.[11][12]



Muslims regard the Qur’an as the main miracle of Muhammad, as proof of his prophethood,[13] and as the culmination of a series of divine messages. These started, according to Islamic belief, with the messages revealed to Adam, regarded in Islam as the first prophet, and continued with the Suhuf Ibrahim (Scrolls of Abraham),[14] the Tawrat (Torah or Pentateuch) of Moses,[15][16] the Zabur (Tehillim or Book of Psalms) of David,[17][18] and the Injil (Gospel) of Jesus.[19][20][21] The Qur'an assumes familiarity with major narratives recounted in Jewish and Christian scriptures, summarizing some, dwelling at length on others, and, in some cases, presenting alternative accounts and interpretations of events.[22][23][24] The Qur'an describes itself as a book of guidance, sometimes offering detailed accounts of specific historical events, and often emphasizing the moral significance of an event over its narrative sequence






Mwanafunzi Arejea kwao


JENNIFER SAMSON [18] mwanafunzi aliyetoroka kwao kutokana na kupata ziro katika matokeo yake ya kidato cha nne arejea nyumbnai kwao jana.
Jennifer alitoweka kwao Januari 30 mwaka huu kwa hofu ya kupewa adhabu na wazazi wake kutokana na kupata ziro katika mitihani yake ya kumaliza elimu ya Sekondari.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kilidai kuwa, Jennifer alirejea kwao hapo majira ya saa 3 usiku, akiwa na hofu kubwa kutokana na kile alichokifanya.

Ilidaiwa kuwa Jennifer aliongozana na mwanamke mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja alioyedaiwa kuwa alikuwa amemuhifadhi nyumbani kwake na alikuja hapo kumuombea msamaha kwa wazazi wake

Hata hivyo ilidaiwa kuwa Jennifer alijieleza kuwa alikuwa nyumbani kwa mama huyo kwa lengo la kumuhifadhi kwa kuwa alikuwa akiwahofia wazazi wake.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alikiri kuwa Jennifer alikuwa nyumbani kwake alimuomba akae kwa muda nyumbani kwake kwa hofu ya wazazi wake



Anga ya Libya huenda ipigwe marufuku


Shirika la kujihami barani Ulaya,NATO pamoja na Washirika wake na Jumuiya ya nchi za Kiarabu zinatafakari hatua za kuthibiti wanajeshi watiifu kwa Kanali Muammar Gaddafi dhidi ya kuendelea kuwashambulia raia.

Kuna mazungumzo ya kupiga marufuku ndege kupaa anga ya Libya kama njia ya kulinda raia na kuwapa nguvu zaidi waasi. Hata hivyo pendekezo hili linaonekana kukumbwa na hatari kadhaa.

Wanadiplomasia kutoka Jumuiya ya Ulaya na Muungano wa Afrika wameunga mkono hatua madhubuti kuchukuliwa dhidi ya utawala wa Libya.





Hali hii ilipelekea baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutangaza vikwazo dhidi ya Kanali Gaddafi na washirika wake wiki jana.Tangu hapo Jumuiya ya nchi za kiarabu zimekua zikitafakari kutangaza marufuku ya ndege kupaa anga ya Libya.

Aidha pendekezo hilo linaungwa mkono na Muungano wa Afrika hasa ikiwa mashambulio dhidi ya raia yakiendelea.Hata hivyo AU imepinga mpango wowote wa kijeshi kutoka nchi za magharibi.






JK aanika mipango ya Chadema







RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametoa tahadhari juu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuwa kinalengo ya kuleta machafuko nchini.
Hayo aliyasema jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi inayorushwa na vyombo vya habari.

Kikwete alisema kuwa chama hicho kinatumia haki ya msingi ya raia ya kufanya maandamano kuchochea vurugu kwa lengo la kuiondoa serikali iliyopo madarakani kimabavu.

Alisema kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria za msingi za kidemokrasia na itaweza kuiweka nchi mahali pabaya ikiwemo na kumwaga damu.

Hivyo aliwataka wananchi kuwa makini na hilo na kutoshawishika na vurugu hizo kwani itaiweika nchi mahali pabaya.
“Kauli za wenzetu za Chadema zinashiria kabisa zinataka vurugu” Kikwete




Umeme na Maji zakatwa Ivory Coast



Afisa wa Umoja wa mataifa nchini Ivory Coast amethibitisha kuwa huduma za maji na umeme zimekatwa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Eneo hio linampinga Laurent Gbagbo, ambaye amekataa kuachia madaraka licha ya jamii ya kimataifa kukubaliana kuwa alishindwa katika uchaguzi wa Novemba mwaka uliopita.

Afisa huyo wa umoja wa mataifa , Ndolamb Ngokwey, amesema kampuni ya umeme ya Ivory Coast imemuarifu kuwa huduma hizo zimekatwa kwa misingi ya kisaisa na hakukua na matatizo ya kimitambo.

Umeme ni muhimu katika eneo hilo la mashambani na hutumika kusambaza maji kutoka kwa mabwawa.






Wapinzani wazuia shambulio la Gaddafi


Kanali Gaddafi


Wapinzani wamepigana kuzuia wanajeshi wanaomtii Kanali Muammar Gaddafi kuuchukua tena mji wa mashariki wa Brega.

Majeshi ya Gaddafi yaliingia katika maeneo ya mashariki kwa mara ya kwanza tangu mji huo uchukuliwe na waandamanaji wiki mbili zilizopita.

Mwandishi wa BBC John Simpson aliyepo Brega anasema wanajeshi wanaomtii Gaddafi hawaonekani kwa sasa mjini humo.

Mapema Kanali Gaddafi alisema kupitia televisheni kuwa "atapigana hadi dakika ya mwisho" na kuonya kuwa maelfu ya wananchi wa Libya watakufa iwapo majeshi ya nchi za Mashariki yataingilia kati.

Mwandishi wetu almefika katika chuo kikuu cha Brega, ambako mapigano makali yalitokea, na inaonekana kuwa wanajeshi wa Gaddafi hawapo kabisa.

Alisema afisa wa juu wa kundi la wanaopinga utawala wa Gaddafi alisema majeshi ya Gaddafi huenda yakawa yameishiwa risasi na kulazimika kurudi nyuma.

Waandamanaji hao wameonekana kufurahia na kujivunia walichofanikisha, anasema mwandishi wetu, na hali katika mji huo ni kama watu wa Kanali Gaddafi hawana hamasa kubwa na kazi wanayoifanya





Chelsea Man U yazua kizaazaa Zambia





Maafisa polisi wanne wameshtakiwa kwa kosa la mauaji baada ya kudaiwa kusababisha vifo vya watu wawili waliokuwa wakitazama mechi ya mpira baina ya timu za Chelsea na Manchester kwenye baa.

Polisi walisema baa hiyo ilikuwa iko wazi kinyume na sheria ikionyesha mechi ya ligi kuu ya soka ya England.

Wateja walikataa kuondoka kwenye baa hiyo na polisi walirusha mabomu ya kutoa machozi katika mji wa Mazabuka kusini mwa nchi hiyo.

Polisi walisema, hali hiyo ilisababisha watu kukurupuka ambapo mwanammke mmoja mwenye umri wa miaka 21 na mwanamme wa miaka 23 walifariki dunia.

Mwandishi wa BBC Mutuna Chanda wa Zambia alisema baa zinaruhusiwa kuwa wazi mpaka saa nne unusu.

Ligi ya England ina ushabiki mkubwa sana Zambia, kama ilivyo kwa nchi nyingine barani Afrika.

Mwandishi wetu alisema kulikuwa na maandamano Mazabuka, kilomita 100 kusini mwa mji mkuu Lusaka, baada ya taarifa kutapakaa siku ya Jumatano juu ya vifo hivyo.

Waandamanaji hao waliziba barabara ya Great North inayounganisha mji ulio maarufu kwa utalii nchini Zambia Livingstone na Lusaka.

Maafisa wa ziada wa polisi walipelekwa mjini humo na hali kwa sasa ni shwari.








UN yamwekea vikwazo Gaddafi


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura - na kupita bila kupingwa - ya kuuwekea vikwazo utawala wa Muammar Gaddafi kutokana na hatua yake ya kutaka kuzima maandamano.
Wajumbe wa UN wakipiga kura ya vikwazo kwa Gaddafi


Baraza hilo limeunga mkono kuweka vikwazo vya silaha na kupiga tanji amana, huku wakifikisha suala hilo katika Mahakama ya Kimataifa (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinaadamu.

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kiongozi huyo wa Libya aondoke madarakani na kuondoka nchini humo.

Serikali ya mpito

Hata hivyo bado anadhibiti mji wa Tripoli, lakini upande wa mashariki wa nchi unashikiliwa na waadamanaji.

Majadiliano ya kuunda serikali ya mpito ya wanaompinga Gaddafi inaarifiwa yanafanyika.

Mustafa Abdel-Jalil, aliyejiuzulu uwaziri wa sheria kwa kupinga matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji amesema tume yenye raia na wanajeshi itaandaa uchaguzi katika kipindi cha miezi mitatu, limekaririwa gazeti binafsi Quryna.


Waandamanaji Benghazi


Mabalozi wa Libya nchini Marekani na katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono mpango huo, ambao unajadiliwa katika mji wa mashariki unaodhibitiwa na waasi wa Benghazi.

Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa zaidi ya watu 1,000 wamekufa, wakati utawala wa Kanali Gaddafi ukijitahidi kuzima vuguvugu la mabadiliko lililodumu kwa siku kumi.

Hii ni mara ya pili tu kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikisha nchi katika ICC, na ni kwa mara ya kwanza kura kama hiyo kupita bila kupingwa.





Maelfu waendelea kukimbia machafuko Libya




Juhudi za kimataifa zinaendelezwa huku maelfu ya watu wakiendelea kwenda kwenye mpaka wa Libya na Tunisia,kukimbia machafuko Libya.Zaidi ya wakimbizi elfu thelathini wengi wao wakiwa raia wa Misri wamekwama.Mwandishi wa BBC anasema hiyo jana zaidi ya watu ellfu kumi na mbili walivuka mpaka.

Katika muda wa wiki moja iliopita watu zaidi ya elfu hamsini wamekimbilia katika eneo la mpaka huo na hakuna dalili kwamba hali hiyo itapungua,wengi wao wakiwa wafanyakazi wa kawaida, raia wa Misri na wanatafuta njia ya kurudi nyumbani.Baadhi yao walipata msaada wa mikate na maji kutoka kwa raia wa Tunisia waliojitolea kuwasaidia.


Huku wengine wakikimbilia kwenye mipaka, mamia ya raia wa kusini mwa jangwa la sahara ni miongoni mwa maelfu ya watu waliopewa msaada wa kutoka nje ya Libya. Raia karibu 500 wa Nigeria waliokuwa Libya waliwasili mjini Abuja jana.

Kwa Gaddafi na familia yake mambo yanazidi kuwa magumu serikali ya Uingereza imezuia mali za Gaddafi nchini humo pamoja na jamii yake na waakilishi wao.Haijulikani thamani yake lakini inasemekana kuwa mamia ya mamilioni ya madola.Hatua hii inafwatia uamuzi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa siku ya jumamosi . Marekani na Uswizi pia tayari wametangaza kusitisha shughuli za biashara kwa makampuni yanayohusiana na kiongozi huyo wa Libya.

Mmoja wa watoto wa kiongozi wa Libya Muammar Gadaffi ameelezea wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa umoja wa mataifa kuwekea jamii ya Gaddafi vikwazo vya kusafiri nje ya nchi.Saadi Gadaffi,aliyekuwa mchezaji mpira wa miguu wa kulipwa na mwanawe Gaddafi wa tatu,amesema maisha yake yote amekuwa akisafiri sana nje ya nchi na sasa itamlazimu atafute huduma za wakili ili aendelee kufanya hivyo.

Katika mahojiano na BBC alieleza hali ilivyo sasa kama tetemeko la ardhi;homa itakayoeneza machafuko na akasema kwamba kama babake ataondoka Libya,nchi hiyo itazama katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe saa moja baada ya babake kuondoka.




Mawaziri wa nje kuijadili Libya


Mawaziri wa mambo ya nje kutoka duniani kote wanakutana mjini Geneva Uswisi, kujadili hatua za kuchukua kukabiliana na janga la kibinaadam linalozidi kukua nchini Libya.
Waandamanaji Libya karibu na picha ya Gaddafi


Maelfu ya wahamiaji, wengi kutoka Misri, wamekwama katika mpaka wa Libya na Tunisia, huku maelfu wakiwasili kila saa, kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa Mataifa.

Waandishi wa habari wanasema kuna hali ya wasiwasi, huku kiongozi Muammar Gaddafi akiendelea kuidhibiti Tripoli.

Wakimbizi kutoka Libya


Marekani imeunga mkono wazi wazi makundi yanayompinga Gaddafi mashariki mwa Libya.

Akifungua mkutano mjini Geneva, Kamishna wa haki za binaadam wa Umoja wa Mataifa Navi Pallay, amezionya mamlaka za Libya kuwa ushambuliaji wa raia unaotapakaa, unaweza kufikia kuwa makosa ya jinai katika sheria za kimataifa.

"Ni suala la masikitiko makubwa kwamba damu imemwagika katika kukaribisha mabadiliko".


Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo kwa Gaddafi


Akizungumza akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema Marekani "inaungana na wananchi wengi wa Libya wa upande wa mashariki".

Bi Clinton amesema atajadili masuala ya kibinaadam na kisiasa na mawaziri wengine kutoka Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika kaskazini katika mkutano wa baraza la haki za binaadam, mjini Geneva.

Watu wasiopungua 1,000 wanadhaniwa kuawa katika wiki mbili za ghasia, ambapo miji ya mashariki imedhibitiwa na majeshi yanayopinga serikali.





Misri yamzuia Bw Mubarak kusafiri





Bw Hosni Mubarak

Mwendesha mashtaka wa Misri ametoa hati ya kumzuia Rais aliyeondoka Hosni Mubarak kusafiri pamoja na familia yake.

Msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka alisema amri hiyo pia inapiga tanji fedha na mali zao.

Bw Mubarak aling'atuka Februari 11, baada ya kukaa madarakani kwa takriban miaka 30, kufuatia kuibuka maandamano yaliyofanywa na umma ukimpinga.

Inaarifiwa kuwa afya yake ni duni, akiishi kwenye nyumba yake ya kifahari huko Sharm el-Sheikh, lakini hajaonekana wala kusikika hadharani tangu alipoachia madaraka.

Alikabidhi uongozi wake kwa jeshi, ambapo iliteua serikali ya mpito itakayoandaa katiba mpya na uchaguzi pia.

Shirika la habari Reuters limeripoti kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka alisema kizuizi hicho cha kusafiri na kupiga tanji mali zake ilitolewa wakati malalamiko yalipotolewa- ambapo haijfafanuliwa- dhidi ya familia ya Bw Mubarak wanachunguzwa.

Misri tayari imeziomba serikali kadhaa kupiga tanji mali za familia ya Bw Mubarak nje ya nchi.

Waandamanaji pamoja na wanaopinga ufisadi wamekuwa wakishinikiza mali za familia ya Bw Mubarak zichunguzwe, ambayo inakadiriwa kuwa kati ya dola za kimarekani bilioni moja hadi bilioni 70.

Hata hivyo, mwakilishi wa kisheria wa Bw Mubarak amekanusha taarifa kuwa aliyekuwa Rais alijilimbikizia mali akiwa madarakani






Waziri mkuu wa Tunisia ajiuzulu




Tunisia
Waziri mkuu wa Tunisia Mohammed Ghannouchi ametangaza kupitia televisheni ya taifa kuwa anajiuzulu- matakwa muhimu kutoka kwa waandamanaji.

Alikuwa akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Tunis, baada ya kutoa hotuba ndefu akijitetea wakati alipokuwa madarakani.

Bw Ghannouchi anaonekana kuwa karibu sana na aliyekuwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali, aliyeondoshwa madarakani mwezi uliopita.

Bw Ghannouchi, mwenye umri wa miaka 69, amekuwa chini ya uongozi wa Bw Ben Ali tangu mwaka 1989.

Alisema, " Baada ya kutafakari kwa zaidi ya wiki moja, nikaanza kushawishika, na familia yangu iliniunga mkono, na hivyo kuamua kujiuzulu. Si kwamba nakimbia majukumu yangu; nimekuwa nikitimiza wajibu wangu tangu Januari 14."

Aliongeza, " Siko tayari kuwa mtu anayechukua uamuzi utakaoishia kusababisha vifo."

"Kujiuzulu huku kutasaidia Tunisa, mapinduzi pamoja na maendeleo ya siku za usoni za Tunisia." Alisema.

Baada ya saa kadhaa mbadala wa Bw Ghannouchi alitajwa- Beji Caid Essebsi, mwenye umri wa miaka 84, ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya marehemu Rais Habib Bourguiba.

Awali, polisi mjini Tunis walirusha mabomu ya kutoa machozi na risasi za onyo kutawanya maandamano ya hivi karibuni wakitoa wito wa kutaka serikali mpya na katiba mpya katika siku ya tatu ya ghasia.





Jaribio la mapinduzi lazimwa Congo


Habari kutoka Kinshasa zinaeleza kuwa watu saba wameuawa baada ya kufanya jaribio la kumpindua Rais Joseph Kabila katika makazi yake.

Watu hao waliuawa na walinzi wa Rais Kabila, kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo.

Mwandishi wetu Lubunga Bya'Ombe akiwa Kinshasa amethibitisha kumetokea taarifa hizo. Hata hivyo watu waliohusika bado hawajajulikana.

Taarifa zaidi tutawaletea kadri zitakavyokuwa zikipatikana





Maandamano zaidi Tunisia



Polisi wamewatawanya waandamanaji katika mji mkuu wa Tunis siku ya Ijumaa wakidai kujiuzulu kwa Mohammed Ghannouchi, ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo baada ya Ben Ali kuikimbia Tunisia mapema mwaka huu.
Waandamanaji nchini Tunisia


Ulikuwa umati mkubwa zaidi tangu Rais Ben Ali kuikimbilia Saudi Arabia mwezi uliopita.

Ben Ali alikuwa Rais wa Tunisia kwa kipindi cha miaka 23 na alitimuliwa baada ya wiki kadhaa za maandamano.

Bw Ghannouchi na serikali yake ya mpito walitangaza wataanda uchaguzi utaofanyika mwezi wa Julai.

Lakini waandamanaji wanaonekana kutoridhishwa na walikuwa wakiimba mitaani 'Ghannouchi ondoka.'

Polisi walifyatua risasi za ilani na mabomu ya kutoa machozi karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Walioshuduia tukio hilo wanasema mtu mmoja tu ndiye aliyejeruhiwa miongoni mwa waandamanaji takriban 100,000.

Bw Ghannouchi aliwahi kufanya kazi katika serikali ya Ben Ali tangu mwaka 1999.





Ubingwa wa Afrika Zamalek yasonga mbele

Zamalek imeingia ngwe ya pili ya kuwania ubingwa wa vilabu barani Afrika, baada ya kuilaza Ulinzi Stars ya Kenya 1-0 mjini Cairo.

Kombe la Caf




Wamisri walioshinda pambano hilo kwa bao la kipindi cha pili lililofungwa na Mahmud Abdel Razek.

Zamalek wamefanikiwa kuingia ngwe ya pili ya mashindano hayo baada ya ushindi wa jumla ya mabao 5-0.

Mpambano huo ulikuwa ufanyike wiki mbili zilizopita, lakini uliahirishwa kutokana na na ghasia za kimapinduzi zilizomuondoa madarakani Rais Hosni Mubarak.

Serikali mjini Cairo iliruhusu mashabiki kuhudhuria mechi hiyo, katika uwanja wa jeshi.

Hiyo ilikuwa ni mechi ya kwanza rasmi kuchezwa mjini Cairo tangu mapinduzi hayo yalipotokea.

Wachezaji wa timu zote mbili walifunga vitambaa vyeusi, kuwakumbuka watu waliopoteza maisha katika vuguvugu hilo maarufu.

Wakati huo huo, Wydad Casablanca ya Morocco pia ilifanikiwa kusonga mbele ngwe ya pili licha ya kufungwa 1-0 na Aduana Stars ya Ghana.

Aduana Stars walikuwa na matumaini ya kulipa deni la kufungwa mabao 3-0 katika mchezo wa awali, wakati Bernard Dong Bortey alipoifungia timu hiyo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 37 na kurejesha matumaini ya kushinda mchezo huo.

Katika michezo mingine mwishoni mwa wiki, AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, iliilaza Ocean View ya Zanzibar3-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-1; JCA Treichville ya Ivory Coast iliilaza AS FAN ya Niger 3-0 na kusonga mbele na ASEC Mimosas, pia ya Ivory Coast iliichabanga ASC SNIM kutoka Mauritania 2-0 na kufanikiwa kusonga mbele raundi ijayo kwa jumla ya mabao 9-0.




Mapigano makali yazuka Somalia


Mapigano yanaendelea nchini Somalia kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa kiislamu wa kundi la Al-Shabab katika mji mkuu Mogadishu na miji mengine.
Wanajeshi wa Somalia katika mazoezi


Mapigano yanaendelea kwa siku ya tatu mfululizo katika mji wa Bula Hawo karibu na mpaka wa Kenya lakini leo yamepungua.

Mji wa Mandera kaskazini mashariki mwa Kenya umepokea watu kutoka Somalia wanaokimbia mapigano hayo ya Bulo Hawo.

Mapigano makali yanaarifiwa kutokea katika maeneo matatu nchini Somalia.

Mwaandishi wa BBC anasema haya ni mapigano makali kabisa kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la wanaharakati wa kiislamu la Al-Shabab, katika mji mkuu, Mogadishu, katika kipindi cha miezi michache iliyopita.

Vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika, inasemekana vimeiteka ngome kuu ya al-Shabaab .

Kuna taarifa za kutokea mapambano katika mji wa Beledweyne kwenye mpaka wa Ethiopia na Bulahawa, na kwenye mpaka na Kenya.


Mpiganaji Somalia
Mapigano makali ya mjini Mogadishu yaliendelea siku nzima Jumatano.

Wanajeshi kutoka Burundi ambao ni sehemu ya jeshi la Muungano wa Afrika wamekuwa wakipigana bega kwa bega na wanajeshi wa serikali hiyo ya mpito ya Somalia.

Wamefanikiwa kuyateka maeneo ya wapiganaji wa Al Shabab baada ya kusonga mbele mtaa kwa mtaa.

Eneo liliotekwa ikiwemo iliyokuwa wizara ya ulinzi ni dogo lakini ni muhimu katika mikakati ya kijeshi.

Kundi la Al Shabab pia limekabiliwa na shinikizo katika mji wa Beledweyne kwenye mkoa wa kati wa Somalia ambako wanajeshi wa serikali na wanamgambo washirika wamekuwa wakifanya mashambulizi.

Katika medani ya tatu ya mapigano Bula Hawo karibu na mpaka wa Kenya wapiganaji wanaohusishwa na kundi la Al Qaeda walishambuliwa na kundi jingine la wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.

Ingawa mpaka huo umefungwa rasmi , wakazi wamekuwa wakikimbia mapigano ya huko na kuelekea mji wa Mandera nchini Kenya.

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed alihutubia waandishi wa habari mjini Mogadishu.

Akiwa amevalia sare ya kijeshi , aliwasifu wanajeshi wa serikali na kusisitiza kwamba mashambulio hayo katika maeneo tofauti yameratibiwa.

Jeshi la Muungano wa Afrika na wanajeshi wa serikali wanazungumzia kuendelea kulivunja nguvu kundi la Al Shabab, hata hivyo kundi hili la msimamo mkali wa kiislamu bado linadhibiti maeneo makubwa ya nchi na linaweza kusababisha vurugu kubwa.

Siku ya Jumatatu bomu liliotegwa ndani ya gari liliwaua watu wasiopungua 17 karibu na kituo cha mafunzo ya polisi mjini Mogadishu.



Carling Cup: Wenger asita kulaumu



Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesita kuwalaumu wachezaji wake baada ya kufungwa 2-1 na Birmingham na kukosa kunyakua Kombe la Carling.
Arsene Wenger


Kuchanganyana kati ya mlinda mlango Wojciech Szczesny na mlinzi Laurent Koscielny, kulimuwezesha Obafemi Martins kuutumbukiza mpira katika nyavu tupu dakika ya 89.

"Kutolewana huko kidogo kumekuwa na athari kubwa katika mchezo na wachezaji wote wawili wamefadhaishwa sana. Simlaumu yeyote," Wenger aliiambia BBC.

"Wakati mambo yakiharibika dakika za mwisho katika mchezo, kunakuwa hakuna muda wa kurekebisha."

Arsenal haijashinda kikombe tangu ilipoilaza Manchester United kwa mikwaju ya penalti kwenye fainali ya Kombe la FA mwaka 2005.

Wenger amekiri kushindwa kuchukua kombe safari hii, ni "jambo gumu sana kulikubali".

Meneja huyo wa the Gunners ameongeza: "Wachezaji wamevunjika moyo, lakini hatuna budi kujizoazoa na hivyo ndivyo timu inatakiwa iwe. Ni nafasi nzuri kuonesha uimara wetu kifikra, jambo ambalo naamini ni muhimu.

"Tumepata kile tulichotarajia kutoka kwa Birmingham. Ni timu inayopigana kiume na kusababisha matatizo mengi makubwa kwa mipira ya mbali.

"Nawapongeza, wamepata kombe, lakini tunasikitika namna tulivyofungwa bao la pili."

Kukataa kwa Wenger kusajili mlinda mlango na mlinzi imara wa kati, kwa mara nyingine kumezua gumzo kufuatia makosa ya mlinzi aliyesajiliwa msimu huu Koscielny, na mlinda mlango Szczesny.






Idhaa za BBC zakamilisha kazi




Ijumaa tarehe 25 Februari 2011, ni siku ambayo itakuwa ya mwisho kwa matangazo ya lugha tano za idhaa za BBC.


Idhaa tano za BBC zafunga kazi
BBC imekuwa ikirusha matangazo kwa lugha ya Ki Serbia tangu mwaka 1939 idhaa ya Yugoslavia ilipoanzishwa. Idhaa hiyo iliendelea hadi mwaka 1991 ilipotenganishwa kati ya Serbia na Coatia kufuatia vita vya huko Balkan.

Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Agosti mwaka 1944, idhaa ya Yugoslavia, baada ya kuanzishwa miaka mitano kabla ilibeba jukumu kubwa la kuwapasha habari takriban watu milioni 20 waliokumbwa na balaa la nchi yao kutekwa na utawala wa Kinazi.

Kazi kubwa ya kuwapasha raia hao habari zisizoegemea upande wowote likawa jukumu la wandishi wa idhaa hiyo, ingawa waliothubutu kuisikiliza walikabiliwa na hatari ya kukamatwa au hata kuuawa.

Idhaa hiyo iliendelea kwa miaka mingine hamsini hadi mwaka 1991, juhudi za Uhuru wa kujitenga ulipozuka huko Slovenia, Croatia na Bosnia.

Hivyo idhaa ya Yugoslania ikagawanywa mara mbili: Serbia na Croatia, ingawa idhaa ya Croatia ilifungwa mnamo mwaka 2005.

Kupitia kipindi kigumu cha muongo wa 1990, wakati serikali ya Slobodan Milosevic ikijitahidi kuziba sauti za vyombo huru, idhaa ya Serbia iliendelea kupeperusha matangazo.

Wasikilizaji wake waliongezeka wakati wa dhiki na matatizo, mfano wakati NATO iliposhambulia Serbia wakati wa vita vya Kosovo.

Hilo huenda lingewafanya raia wa Serb waichukie serikali ya Uingereza kwa kuongoza mashambulio hayo lakini wasikilizaji wa idhaa ya Serb waliendelea kuisikiliza.

Zaidi ya miaka kumi tangu Milosevic apinduliwe, Taifa imara la Serbia yenye utawala unaofuata demokrasia limejitokeza likijitahidi kuwmwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Hoja ni kwamba umuhimu wa kuhitaji idhaa ya lugha ya Ki-Serb umepungua kutokana na kwamba nchi hiyo imejenga vyombo vyake vya utangazaji na habari pamoja na taasisi za kutegemewa.

Hivyo basi, baada ya huduma ya miaka 72 tangu BBC ianze kupeperuha matangazo yake kwa lugha ya Wa-Serb wenyewe, matangazo hayo yamesikika kwa mara ya mwisho leo ijumaa tarehe 25 mwezi wa pili mwaka 2011 na nchi nzima inaiaga BBC na idhaa ya Kiserb iliyowahudumia kupitia vipindi vigumu katika historia ya eneo hilo.

Kwa upande mwingine majirani wa wa Swahili barani Afrika, na ofisini, Wareno wanaopeperusha matangazo yao Afrika, wakiwa na wasikilizaji milioni moja na nusu nchini Msumbiji peke yake, walianza matangazo yao mnamo mwaka 1930 na kukata matangazo hayo alfajiri ya ijumaa tareh 25 mwezi febuari mwaka 2011.

Licha ya kufunga matangazo ya Rediyo, idhaa hiyo ijukanayo kama BBC Mundo itaendelea kujenga mawasiliano yake kupitia tovuti.

Idhaa ya BBC ya matangazo ya dunia inasema imechukuwa uwamuzi mgumu wa kufunga idhaa hizo kutokana na uwamuzi wa kupunguza matumizi kama ilivyotakiwa na serikali.







Assange kufikishwa Sweden
Assange


Jaji katika mahakama moja kusini mwa mji wa London, Uingereza, ameamua kwamba mwanzilishi wa tovuti ya WikiLeaks, inafaa afikishwa nchini Sweden, kwa mashtaka dhidi ya ubakaji.


Assange anasema utaratibu unaotumia kuwasafirisha watuhumiwa Ulaya haufai
Hata hivyo Julian Assange anakanusha mashtaka hayo.

Wakili wake amesema watakata rufaa kuhusu uamuzi uliopitishwa Alhamisi.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo, Bw Assange amesema utaratibu wa kuwahamisha washtakiwa barani Ulaya kutoka nchi moja hadi nyingine unafaa kuchunguzwa upya.