KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Ukitaka Kuoa Nchi Hii Lazima Umnunulie Mwanamke Nyumba


Wanaume wote raia wa kigeni watakaotaka kuwaoa wanawake wa nchini Tajikistan watalazimika kuzifungua waleti zao na kuwanunulia nyumba wake zao kabla ya ndoa kwa mujibu wa sheria mpya iliyopitishwa na bunge la nchi hiyo leo.
Kuanzia leo mwanaume yeyote ambaye si raia wa Tajikistan ambayo zamani ilikuwa sehemu ya Urusi, atalazimika kumnunulia nyumba mwanamke anayetaka kumuoa kama sharti kubwa la kwanza kabla ya harusi.

Hiyo ni kwa mujibu wa sheria mpya iliyopitishwa leo na bunge la nchi hiyo ambapo sharti kubwa lingine lililopitishwa ni kwamba mwanaume atalazimika kukaa mwaka mmoja nchini humo kabla ya kupewa kibali cha kuruhusiwa kuoa.

Watunga sheria wa Tajikistan wamesema kuwa sheria hiyo mpya itasaidia kuwalinda wanawake wanaotelekezwa na waume zao raia wa kigeni.

"Baada ya ndoa kuvunjika, majukumu ya kuwalea watoto huangukia kwa mama na serikali", alisema mwakilishi wa rais bungeni, Dzhumakhon Davlatov.

Davlatov aliongeza kuwa kupitishwa kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza idadi ya wanaume watakaowatekeleza wake na watoto wao.

Wanaume wengi toka Afghanistan na Iran, ndio wanaoongoza kwa kuoa wanawake wa Tajikistan ingawa katika miezi ya karibuni kumekuwa na ongezeko la wanaume wengi toka nchi za barani ulaya, Marekani na Japan wanaooa wanawake wa Tajikistan.

Tajikistan ni nchi maskini iliyokuwa miongoni mwa nchi zilizounda Umoja wa Sovieti na uchumi wake umetetereka tangu mwaka 1990 kutokana na matatizo ya kisiasa na vita vya wenyewe kwa wenyewe

No comments:

Post a Comment