KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Mtunza Maiti Mwananyamala Aisaidia Polisi


MTUNZA maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mwananyama anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano kuhusiana na sakata la kufukiwa kwa maiti za vichanga kumi waliokufa hospitalini hapo.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema wanamshikilia mtunza maiti wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo kwa mahojiano.

Mbali na mtunza maiti huyo pia jeshi hilo linamshikilia Nesi aliyekuwa zamu wakati tukio hilo lilipotokea hospitalini hapo.

Serikali mkoani Kinondoni imeunda tume ya watu watano wakiwemo na madaktari wa hospitali hiyo.

Hata hivyo imedaiwa kuwa baadhi ya wazazi walikabidhiwa maiti hizo na tukio hilo kudaiwa mkono wa wazazi kuhusika na tukio hilo kwa kuwa vichanga vitatu vilikutwa na majina ya wazazi wao kwenye plasta zao za mikononi.

Jeshi la plisi kwa kushirikiana na uongozi Kinondoni bado wanaendelea na uchunguzi wa kina na kubaini wahalifu waliouhusika katika tukio hilo.

Vichanga hivyo vilikutwa vimezikwa maeneo ya Mwananyamala Kwa Msisiri pembezoni mwa makaburi ya Kwa Kopa.

Vichanga hivyo vipatavyo kumi vilikuwa vimeviringishwa katika shuka moja lenye nembo ya hospitali hiyo na kuzikwa katika shimo moja lenye urefu futi moja na nusu

No comments:

Post a Comment