KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, January 12, 2011
Kura Sudan kusini yaashiria kujitawala
Uhesabuji kura ukifanyika Juba
Matokeo ya awali ya kura za maoni kutoka Sudan kusini yanaashiria eneo hilo limepiga kura nyingi kuunga mkono kujitenga kutoka kaskazini na kuunda nchi mpya.
Matokeo kamili yanatarajiwa kutoka mwezi ujao, lakini mji huo unatarajiwa kwa hali ya juu kujitenga.
Raia wa Sudan kusini waishio Ulaya tayari wamepiga kura kwa asilimia 97 wakiunga mkono kuundwa kwa taifa jipya.
Kura hii ya maoni ya kihistoria ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya amani iliyotiwa saini na Sudan kaskazini mwaka 2005, yakimaliza miongo kadhaa ya vita.
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa Januari 9 na kufungwa rasmi siku ya Jumamosi jioni.
Ilitakiwa angalau aslimia 60 ya wapiga kura kujitokeza ili kura hiyo iidhinishwe rasmi, lengo ambalo lilifikiwa kwa urahisi katikati ya juma.
Mwenyekiti wa tume ya kura ya maoni ya Sudan kusini, Mohamed Ibrahim Khalil, alisema zaidi ya asilimia 80 ya wapiga kura wenye sifa za kupiga upande wa kusini walipiga kura hiyo, huku asilimia 53 kutoka kaskazini na asilimia 91 ya wapiga kura wanaoishi katika nchi nane ambapo vituo vya kupigia kura vimewekwa.
Alisema kura hiyo ya maoni itachukuliwa kama "matokeo mazuri katika kiwango chochote cha kimataifa".
Raia wa Sudan kusini wanaoishi Australia wamepewa muda wa ziada wa kupiga kura ambapo mafuriko yalivuruga shughuli hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment