KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Cameron atetea utamaduni wa kimagharibi

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema nchi yake inapaswa kuweka kando mfumo ulioshindwa wa kuhimiza utamaduni mchanganyiko na badala yake ametetea kwa nguvu zake zote utamaduni wa kimagharibi.

Katika hutuba iliyoandaliwa kwa ajili ya mkutano wa amani utakaofanyika mjini Munich nchini Ujerumani, Bw Cameron ameonya kuwavumilia wale wanaopinga usawa na demokrasia na kuhimiza kutengana kunochochea kuongezeka kwa imani zenye itikadi kali.

Ametoa wito kwa serikali mbali mbali kupambana na aina yoyote ya mfumo wa itikadi kali, kwa mfano kusitisha ufadhili kwa makundi ya Kiislam hata kama hayatetei ghasia,

Matamshi ya Bw Cameron yanafanana na hutuba iliyotolewa na Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel, ambaye mwaka uliopita alisema mfumo wa utamaduni mchanganyiko ulikufa.

No comments:

Post a Comment