KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Bomu laua raia tisa Afghanistan



Basi lililolipuliwa

Bomu lililotegwa barabarani limeua raia tisa amabo walikuwa wakielekea kwenye harusi kaskazini mwa Afghanistan.

Watu hao walikuwa wakisafiri kwenye jimbo la Baghlan basi lao lililpoharibiwa.

Waathirika wa bomu hilo ni mtoto, wanawake watatu na wanaume wawili.

Siku ya Jumamosi, bomu jingine lililokuwa limetegwa barabarani liliua watu sita katika wilaya ya Sangin.

Watu wengine watatu walijeruhiwa kutokana na mlipuko huo.

Walipuaji walikuwa wanalenga gari la polisi lakini kama ilivyo kawaida, raia ndio walioathirika.

Wiki mbili zilizopita watu kumi na wanne waliuwawa katika eneo hilo wakati bomu lililipuwa gari lao.

Mara kwa mara mashambulio hutekelezwa katika barabara za Afghanistan, hususan kusini mwa nchi hiyo, na raia ndio waathirika kila wakati.

Idadi kubwa ya watu waliuwawa mwaka jana ambapo zaidi ya watu 2400 walifariki dunia kupitia mashambulio ya bomu zilizotegwa.

No comments:

Post a Comment