KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Watoto wa waliotekwa nyara waachiliwa huru.Watoto wote 20 wa shule moja ya chekechea mjini Paris pamoja na mwalimu wao wameachiliwa bila ya tukio lolote, baada ya kutekwa nyara na kijana mmoja aliyekuwa amejihami kwa mapanga mawili. Tukio hilo katika mji wa Besancon, mashariki mwa
Ufaransa lilitokea jana asubuhi. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 kwanza aliwaachilia kwa hiari mateka wengi,
lakini akabaki amewazuia wanafunzi watano pamoja na mwalimu wao.

Baadaye polisi waliingia ndani ya jengo hilo na kumshawishi kijana huyo awaachie huru mateka waliosalia, na kisha wakamkamata. Kijana huyo anasemekana anakabiliwa na tatizo la kusononeka

No comments:

Post a Comment