KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, December 10, 2010

Viongozi Wasiotekeleza Ahadi Kuwajibishwa


WANAWAKE wa vijiji 40 katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro
wamesema watawawajibisha viongozi ambao watashindwa kutekeleza ahadi
za maendeleo walizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu
uliofanyika mwaka huu.
Wanawake hao walisema kuwa walizisikia ahadi za wagombea kupitia mikutano ya hadhara na radio zinazotumia nishati ya jua au betri zilizotolewa na UNIFEM.

Kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, UNIFEM ilitoa radio 400 aina ya Dynamo ambazo ziligawiwa kwa wanawake kwenye maboma ya Wamasai katika maeneo kadhaa ya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Monduli na Longido mkoani Arusha na Same mkoani Kilimanjaro.

Radio hizo zilitolewa ili kuwezesha jamii zilizoko pembezoni hasa wanawake kuweza kupata habari za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu na masuala ya maendeleo kwa ujumla.

Baadhi ya wanawake wa Kimasai walionufaika na radio hizo wamesema
taarifa wanazozipata kupitia radio zimewatoa gizani, kwani tofauti na
miaka iliyopita mwaka huu waliweza kufuatilia habari za uchaguzi na
habari nyingine nyingi kupitia radio hizo.

“Hata baraza la mawaziri lililoteuliwa na rais hivi karibuni tumelisikia vizuri na kujua matarajio yao katika kuongoza Tanzania yetu,” alisema Elena Kalembu, mkazi wa Oltepesy Loliondo.

Katika mpango huo vijiji vilivyonufaika na radio hizo ni Terrat, Orkaria, Loiborsiret, Lemkuta A, Naberera, Loiborsoit, Lemkuta B, Ormanie, Loondelemati A, Loondelemati B, Shuleni, Sabasaba, Mlimani, Ngarashi, Lendikinya, Madukani B, Emboreet, Madukani A na Lorng`oswani.

Vingine ni Naiti, Nanja, Mbuyuni, Lambo, Orkisima, Mti mmoja, Loolera, Njaro, Barabarabi, Loodo Lorkaria, Karatin, Lepurko, Arkatan wakati huko Same ni vijiji vya Emuguru, Olmaroroi, Lendikinya, Murandawa, Engutoto na Kosiki

No comments:

Post a Comment