KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

..UN: Ouattara ndiye mshindi Ivory Coast

Wananchi wa Ivory Coast wakizungumzia mzozo wa kisiasa nchini mwao. Jamii ya kimataifa yasema kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara ndiye aliyeshinda na wala sio Rais wa sasa Laurent Gbagbo

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limetoa taarifa inayomwidhinisha kiongozi wa upinzani nchini Ivory Coast, Alassane Ouattara kuwa ndiye aliyeshinda kura ya urais -- na wala sio rais wa sasa, Laurent Gbagbo, ambaye amejaribu kujitangaza mwenyewe kuwa mshindi.


Awali Urusi ilikuwa imeelezea wasiwasi kwamba kwa kumtangaza bwana Ouattara mshindi, umoja wa mataifa utakuwa umezidisha majukumu yake.

Uamuzi wa baraza hilo uliokumbwa na pingamizi kutoka kwa Urusi sasa umeimarisha shutuma za kimataifa dhidi ya rais Laurent Gbagbo, ambaye ameendelea kupuuza wito wa jamii ya kimataifa wa kumtaka ajiondoe madarakani.

Jana Jumatano, afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast, Choi Young-jin, amesema tathmini yake ya matokeo ya uchaguzi imemshawishi kwamba wapiga kura walimchagua bwana Ouattara kama rai bila pingamizi yoyote.

Awali serikali ya bwana Gbagbo ilpuuzilia mbali wito kutoka kwa jumuiya ya kiuchumi kwa mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS, wa kumtaka ajiondoe madarakani.

Juhudi za umoja wa Afrika, AU za kujaribu kutatua mgogoro huo kupitia rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki hazijaonekana kupata mafanikio ya haraka

No comments:

Post a Comment