KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

Ufisadi ndio unaozungumziwa sana duniani



Umaskini umewasukuma wengi kuombaomba barabarani nchini Uzbekistan. Lakini swala hili halizungumuziwi sana kama ufisadi duniani.
Kura ya maoni ya kimataifa iliyofanywa na BBC imeashiria kuwa ufisadi miongoni mwa maafisa wa serikali ni mojawepo wa matatizo yanayozungumziwa sana duniani.

Uchunguzi huo umebaini kuwa hongo, ufisadi na ulafi miongoni mwa maafisa wa serikali ulijadiliwa sana miongoni mwa marafiki na watu wa familia moja kuliko swala la mabadiliko ya hali ya anga, umaskini, ukosefu wa ajira na hata ongezeko la bei ya vyakula na kawi.

Kura hiyo ya maoni ya BBC iliwahusisha watu alfu 13,000 kutoka mataifa 26. Asilimia 21-takriban mtu mmoja kati ya watano waliohojiwa- walisema wamejadili maswala kuhusu ufisadi na ulafi na marafiki au watu wa jamii yao katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita


Maadhimisho ya siku ya ufisadi duniani mjini Jarkata, Indonesia.
Hali hiyo imefanya ufisadi kuwa tatizo la dunia linalozungumziwa sana. Swali tofauti lililoulizwa na BBC liliwataka watu kukadiria ni maswala gani waliozingatia kuwa yenye umuhimu mkubwa yanayopaswa kushughulikiwa kwa dharura.

Ufisadi ulishika nafasi ya pili kama mada yenye umuhimu mkubwa baada ya umaskini.

Wale waliohojiwa nchini Brazil, Misri, Colombia, Ufilipino na Kenya walizingatia zaidi ufisadi kuwa ndio tatizo kubwa duniani.

Barani Ulaya, raia wa Italia ndio waliolezea zaidi wasiwasi wao kuhusu ulaji rushwa.

Uchapishaji wa matokeo ya utafiti huo wa BBC unasadifiana na maadhimisho ya siku ya ufisadi duniani inayoongoozwa na Umoja wa Mataifa leo Alhamisi.

No comments:

Post a Comment