KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Theluji yatatiza usafiri Ujerumani
Usafiri umetatizwa katika maeneo kadhaa hapa Ujerumani, kutokana na kuanguka kwa theluji nyingi. Pia inaripotiwa kumetokea ajali kadhaa barabarani, baadhi ya viwanja vya ndege vimefungwa na usafiri wa treni kutatizwa. Watu wawili wanaripotiwa kufariki katika ajali ya barabarani, huku viwanja vya ndege vya Frankfurt, Stuttgart, Dusseldorf na Cologne vikifungwa na safari nyingi kufutwa. Idara ya hali ya hewa hapa Ujerumani imetabiri kuwa theluji itazidi kuanguka katika maeneo mengi hapa Ujerumani hii leo kesho na pia Jumapili

No comments:

Post a Comment