KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

SPLM yaunga mkono uhuru wa kusini

Chama tawala cha Sudan Kusini - SPLM - kwa mara ya kwanza kimetamka hadharani kuwa kinaunga mkono uhuru wa upande wa kusini, kabla ya kura ya maoni kupigwa mwezi ujao, kuhusu suala hilo.


Jinsi Sudan itakavyogawanyika iwapo kusini watajitenga




Taarifa hiyo ni kinyume na makubaliano ya mkataba wa amani wa mwaka 2005 uliomaliza miaka mingi ya vita vya wenywe kwa wenyewe, dhidi ya Sudan Kaskazini.

Katika mkataba huo, SPLM na chama kinachotawala upande wa kaskazini NCP walikubaliana kushirikiana kujenga umoja.

Lakini afisa wa ngazi ya juu wa SPLM amesema NCP imefanya umoja kuonekana sio wa kuvutia.

Kura ya kujitenga na kuungana Sudan


Afisa huyo Anne Itto alisema SPLM sasa kitafanya kampeni ya kuigawa nchi. "Kwa kuwa umoja umefanywa kuonekana sio wa kuvutia, hivi sasa tunapigia kampeni kile watu wetu walichochagua, kwa sababu tunafuata matakwa ya watu," amesema.

Ameweka wazi kuwa anazungumza kwa niaba ya chama upande wa kusini, na sio kikundi kidogo cha upande wa kaskazini.

Mwandishi wa BBC James Copnall aliyepo katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum amesema kasi ya upande wa kusini kutaka kujitawala haizuiliki. Amesema hakuna makubwa yaliyofanywa na kundi la zamani la waasi SPLM au NCP kuonesha kuwa umoja ni kitu cha kuvutia.

Mvutano ni mkubwa wakati huu wa kuelekea kwenye kura ya maoni, huku SPLM ikituhumu upande wa kusini kwa mashambulio madogo madogo dhidi ya kusini, wakati jeshi upande wa kakazini ukikana madai hayo


Wananchi wa Sudan


Katika tukio jingine tofauti, mtu ambaye anahusika na kuandaa kura ya maoni upande wa kusini, Mohammed Ibrahim Khalil ameonya kuwa wapinzani wa kura hiyo wanajaribu kukwaza shughuli hiyo kwa kuweka pingamizi za kisheria.

"Wazo ni kuzusha mkanganyiko na kuonesha watu kuwa kuna jambo linaenda mrama," amesema.

Hata hivyo amegoma kusema ni nani anadhani anahusika na kampeni ya kuleta rabsha.

No comments:

Post a Comment