KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, December 10, 2010

Somali: Kenya yapondwa tena na Amnesty

Wakimbizi kutoka Somalia. Amnesty International inasema Kenya inaendelea kuwahangaisha raia wa Somalia wanaokimbia mapigano pamoja na msukosuko wa kisiasa nchini mwao


Shirika la Amnesty International limekosoa jinsi serikali ya Kenya inavyowahangaisha wakimbizi kutoka Somalia wanaoishi nchini humo.

Ripoti mpya ya shirika hilo inasema wasomali wanaokimbia mapigano pamoja na msukosuko wa kisiasa nyumbani kwao wananyanyaswa na maafisa wa polisi nchini Kenya.

Wanawake na watoto wanaokimbia mapigano nchini Somalia wapiga foleni kujiandikisha katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kaskazini mwa Kenya.Ripoti hiyo inasema kuwa wasomali wanakumbana pia na changamoto za kiusalama katika kambi za wakimbizi zilizofurika , ambako wanalengwa kupelekwa vitani na vikosi vya kenya pamoja na kundi la wanamgambo wa kiislamu la al-Shabaab.

Hapo awali serikali ya Kenya imewahi kukanusha shutuma za kuhusika katika kuwatesa wakimbizi wa Somalia.

Mapema juma hili, polisi nchini Kenya waliwatia nguvuni zaidi ya watu mia moja sitini wenye asili ya Somalia katika vitongoji vya mji wa Nairobi na kuwashtaka kwa kosa la kuwa nchini humo kinyume na sheria

No comments:

Post a Comment