KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, December 22, 2010

Simba Mbioni Kumtwaa Nyota wa Ivory Coast


VIONGOZI wa Simba wamekuwa wakihaha kuona namna nzuri kama wanaweza kumsajili mshambuliaji hatari wa Ivory Coast, Kone Zoumana baada ya kufurahishwa kwao na kiwango chake.
Mchezaji huyo ndiye mfungaji wa bao la kufutia machozi wakati miamba hiyo ya Magharibi ilipoumana na Rwanda katika mchezo wa kuwania Kombe la Chalenji uliochezwa Uwanja wa Taifa mwishoni mwa mwezi uliopita. Rwanda ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1.

Ivory Coast, Malawi na Zambia zilishiriki michuano hiyo inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka vya Nchi za Afrika Mashariki na Kati, CECAFA, iliyofanyika jijini Dar es Salaam wakiwa kama timu zilizoalikwa.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, mmoja wa kiongozi wa Simba aliye katika Kamati ya Usajili alionekana kumfuatilia kwa karibu mchazaji huyo.

Baadaye, kiongozi huyo alimvaa meneja wa timu hiyo akijaribu kupata mawasiliano ya karibu ya mchezaji huyo huku akiulizia kama wanaweza kupata saini yake.

Kiongozi huyo alipoulizwa kuhusiana na habari hii aligoma kuzungumzia suala hilo kwa kudai kwamba bado ni mapema kwa sasa.

"Bado ni mapema, lakini kumbuka nafasi za wachezaji wa kigeni zimejaa ingawa tumevutiwa naye na ndio maana tunajaribu kupata contact yake,"

"Ninachokifanya kwa sasa ni kumfuatilia kwa karibu kabla sijapeleka ripoti kwa wahusika (kocha na benchi la ufundi kwa maamuzi mengine," alisema.

No comments:

Post a Comment