KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Polisi ‘wapika dawa’ ya utekaji magari

Festo Polea
JESHI la polisi nchini limesema linatarajia kuweka ulinzi mkali kwenye barabara kuu nchini kukomesha matukio ya utekaji magari, uporaji mali na udhalilishaji abiria.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Said Mwema, alisema mradi huo unaogharimu dola za Marekani 1.8 milioni, utekelezaji utaanza kwenye barabara ya Dar es Salaam-Rusumo/Kagera.

Mwema alikuwa akizungumza wakati wa kutia saini mkataba na Taasisi ya Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji (ICF), unaohusu mradi wa ufadhili wa usimamizi barabara kuu ili kuboresha usalama barabarani.


Alisema ulinzi utaimarika kila kituo na mitambo maalumu ya kompyuta itatumika kukagua magari yatayopita kwenye njia hiyo.
“Tunachotaka kuwa, ni jeshi la kisasa lenye weredi na kushirikiana na jamii, hivyo askari wetu wamepata mafunzo ya kukabiliana na matukio ya barabarani, wakati wengine wakiwa barabarani wenzao watakuwa vituo maalum wakifuatilia magari yote yanayopita barabara hiyo,” alisema Mwema na kuongeza:




“Lengo ni kutokuwa na udanganyifu wa kupitisha mizigo bandia na yenye kuhatarisha usalama na barabara zetu.’’
Aliongeza kuwa iwapo mradi huo unaoshirikisha taasisi mbalimbali zikiwamo, TRA, Tanroads, Tatoa, Sumatra na mengineyo utafanikiwa, itaongeza uwekezaji ndani ya nchi na ICF kwenye barabara zote kuu.

“Mradi huu kwetu ni kama tone la damu kwenye bahari kwa kuwa, utekelezaji wake hautakuwa na sababu ya polisi kusimamisha magari kwa ukaguzi kila kituo, bali kupitia mfumo wa kompyuta kutakuwa na takwimu maalum,’’ alisema Mwema.
Naye Mtendaji Mkuu wa ICF, Omary Issa, alisema mradi huo utaondoa nyanja zote za upitishaji mizigo bila kugaguliwa na kwamba, ulinzi utaimarika mizigo itafika kwa wakati na abiria watafika salama.
Issa alisema kutokana na kutumika kwa mfumo wa kompyuta, wakaguzi watakuwa na takwimu zote za magari toka Dar es Salaam -Lusumo/Kagera

No comments:

Post a Comment