KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, December 10, 2010

Mvua Yaharibu Nyumba 20 za Polisi Songea


NYUMBA 20 zimeezuliwa mapaa likiwemo jengo la ofisi za elimu, zimamoto na kambi ya nyumba za askari polisi zilizopo kwenye manispaa ya Songea baada ya mvua kubwa iliyoambatana na radi kunyesha.
NYUMBA 20 zimeezuliwa mapaa likiwemo jengo la ofisi za elimu, zimamoto
na kambi ya nyumba za askari polisi zilizopo kwenye manispaa ya Songea
baada ya mvua kubwa iliyoambatana na radi kunyesha.

Akizungumza na waandishi wa habari kambini hapo alipokwenda kwa lengo
la kuwafariji, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamuhanda, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mvua hiyo imeleta maafa kwa kuezua nyumba tatu wanazoishi askari polisi na kuharibu vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 12.

Alisema familia zilizoathirika na mvua hiyo zimepatiwa makazi kwenye kambi nyingine ya askari wa kituo cha kutuliza ghasia (FFU) wakati tathmini kamili ya maafa hayo ikiendelea kufanyiwa uchunguzi.

Kamanda huyo alisema, nyumba zingine za raia zimeharibiwa vibaya na mvua hiyo huku akiongeza kuwa jeshi lake linaendelea kutoa msaada kwa familia zilizohusika huku wakisubiri kupata tathmini kamili.

Kwa upande wake, Ofisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Songea, Jamuhuri Kidumu, alisema mvua hizo zimeleta madhara kwa kompyuta na nyaraka nyingine za serikali ambazo hadi sasa thamani yake haijafahamika.

“Mafaili ya walimu wa sekondari na shule za msingi waliokuwa wanaandaliwa malipo yao ya likizo kwa ajili ya Desemba yameharibiwa vibaya na mvua, hivyo inabidi taratibu zianze upya ili kuwalipa walimu hao,” alisema Kidumu

No comments:

Post a Comment