KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

Museveni ahofia kupinduliwa na Ghadhafi


Gazeti linalochapishwa nchini Uingereza la Guardian limechapisha risala za wanabalozi kutoka Balozi za Marekani kutoka sehemu mbalimbali za Afrika.

Yaliyochapishwa na gazeti hilo ni matukio ya hivi karibuni kutoka ujumbe wa siri za Marekani uliovuja kupitia shirika la Wikileaks na kusababisha mizozo ya kisheria na kisiasa baina ya wakuu wa Marekani na mtandao huo.

Kurasa zilizovuja ni kuhusu masuala ya ndani ya Afrika, kama yalivyochapishwa na gazeti la Guardian, yakiwa matamshi ya wanabalozi za Marekani walioko Uganda, Kenya ,nigeria na Eritrea.



Masuala mengi yaliyovuja yanafahamika na waafrika wengi wenye ufahamu wa mambo, lakini uhondo na uhakika umo katika nakala sahihi za matamshi.

Bila shaka inafahamika kuwa kwa mda mrefu Marekani imekuwa ikitowa msaada wa kijeshi kwa serikali ya Uganda - sababu kubwa ikiwa kukabiliana na tishio la serikali ya kiislamu katika nchi jirani ya Sudan.


Rais Museveni aliwambia wa Marekani kuwa ana wasiwasi huenda Ghadhafi akaindungua ndege yake.

Ingawaje hayo yalielezewa hivyo lakini la kushangaza ni kufahamu kwamba Balozi wa Marekani mjini Kampala aliarifu kupitia mawasiliano na wakuu wa Marekani kuwa Uganda inaelewa vyema umuhimu wa kushauriana na Marekani endapo itaibidi kuendesha vita nje ya utaratibu wa sheria, au kwa maelezo ya kawaida, labda kutenda uhalifu katika vita.

Nchini Kenya, vitendo vya kihalifu vinavyoendeshwa na serikali hujadiliwa bayana katika magazeti na inashangaza kusoma kuwa Mwanabalozi wa Marekani akisema kuwa polisi wa ngazi ya juu ana uhusiano na kundi moja linalohusika na mauwaji.

Nchini Nigeria si ajabu wala siri kuwa makampuni ya mafuta yana ushawishi mkubwa katika serikali, lakini maoni ya Ubalozi wa Marekani na Kampuni ya Shell kuhusu masuala nyeti ni ya kushangaza.

Waraka kutoka kwa Balozi wa Marekani nchini Eritrea unatoa onyo kali kwa nchi hiyo dhidi ya uhusiano wake na makundi ya Kiislamu yaliyo katika nchi jirani ya Somalia.

Mjumbe wa Marekani anatoa dhana yake juu ya kile anachokitaja kama uwezekano wa shambulio kubwa la magaidi wa Kisomali dhidi ya Marekani, na kuitaka Eritrea itafakari, ikizingatia historia ya hivi karibuni, ni jinsi gani Marekani itajibu kitendo cha aina hiyo

No comments:

Post a Comment