KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Mti wa Krismasi kwa waasi wa Colombia



Wanamgambo wa FARC nchini Colombia.


Jeshi la Colombia limesema kuwa limeweka mti mkubwa wa Krismasi katika eneo linalothibitiwa na kundi la waasi la FARC ili kuwashawishi wapiganaji wa kundi hilo kuweka silaha chini.

Wanajeshi wa serikali waliingia katika eneo hilo la mlima wa Macarena ambalo haliwezi kufikika kwa urahisi na kuupamba mti huo wa Krismasi ulio na urefu wa mita ishirini na tano na kuweka takriban taa za umeme alfu mbili zinazometameta.



Mti wa Krismasi
Jeshi la Colombia linasema litaweka miti zaidi katika maeneo mengine yanayokaliwa na kundi hilo la waasi ili kutoa ujumbe kwa wapiganaji hao kwamba siku kuu ya Krismasi ni siku mwafaka ya kuachana na vita.

Serikali ya Colombia inasema kuwa zaidi ya wapiganaji alfu mbili wa kundi hilo la waasi waliweka silaha chini mwaka huu kupitia mpango wa kuwapa msamaha na kuwasaidia kurejea katika maisha ya uraia.

No comments:

Post a Comment