KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Mlipuko Afghanistan yasababisha vifo

Raia kumi na wanne wamefariki dunia baada ya basi kulipuliwa na wanamgambo katika barabara kuu inayotoka Herat ikielekea Kandahar.

Msemaji wa gavana wa eneo hilo amesema kuwa wanawake na watoto walikuwa miongoni wa walioaga dunia.

Inaarifiwa kuwa watu wengine wengi zaidi wamajeruhiwa.



Basi hiyo ilikuwa ilkuwa imejaa wasafiri waliokuwa wakielekea Kandahar asubuhi mapema.


Basi lililolipuliwa hivi karibuni, Afghanistan


Mashambulio hutekelezwa barabarani mara kwa mara na kufanya barabara kuwa eneo la vita.

Serikali na vikosi vya muungano zinajaribu kutengeneza barabara kuu zinazoweza kupitika lakini Taleban bado inaendelea kutekeleza mashambulio.

Rais Karzai amesema shambulio hilo ni kinyume na maadili ya kiislamu na alituma rambirambi zake kwa familia za waliofiwa.

Mapema mwezi huu raia kumi na wanne wa Afghanistan waliuwawa walipokuwa wakienda kuhudhuria sherehe za harusi magharibi mwa nchi hiyo.

Kama tukio la hivi karibuni, pia wao basi lao lillipuliwa na bomu lililotegwa kando ya barabara hiyo

No comments:

Post a Comment