KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

Mgao wa Umeme na Dili la Majenereta


MGAO wa Umeme unaoendelea katika mikoa mbalimbali hapa nchini umechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa wafanyabiashara kadhaa wanatumia janga hilo kuingiza majenereta feki yanayobandikwa nembo za makampuni makubwa duniani.
MGAO wa Umeme unaoendelea nchini umechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa wafanyabiashara kadhaa wanatumia janga hilo kuingiza majenereta ambayo hayana viwango vinavyokubalika hapa nchini.

Uchunguzi wa kina umebaini kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wakibandika nembo za makampuni makubwa duniani katika bidhaa wanazouza yakiwemo majenereta, hali inayodaiwa kusababishwa na baadhi ya asasi husika kutokuwa makini katika utendaji wao wa kazi.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa nyingi kati ya bidhaa hizo hasa zile za umeme zinazotoka nje ya nchi ni bandia na ambazo zimekuwa zikichangia kulipuka na kusababisha majanga makubwa ya moto, na kwamba kuingia kwake nchini kumeshamiri katika kipindi hiki ambacho taifa liko kwenye mgao wa umeme.

Kwa kina kabisa mwandishi wa habari hizi amefanya uchunguzi na kugundua kuwa maduka makubwa kadhaa yaliyoko katikati ya Jiji la Dares Salaam yamekuwa yakiuza bidhaa za umeme yakiwemo majenereta ambayo kiwango chake kinatia mashaka.

Imedaiwa kuwa wamiliki wa maduka hayo wamekuwa wakindika nembo na stika za makampuni makubwa yanayozalisha bidhaa zenye ubora, ili kuhadaa umma kuhusiana na bidhaa hizo feki zinazouzwa katika maduka yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Triple H Trading inayouza bidhaa za umeme yakiwemo majenereta alikiri kuwapo kwa wafanyabiashara wanaoingiza nchini bidhaa feki na kwamba ndiyo wanaochangia kuwakosesha imani wanunuzi nchini.

Alikuwa akijibu madai ya baadhi ya watumiaji kwamba baadhi ya makampuni makubwa yamekuwa yakibandika nembo za makampuni makubwa huku yakiuza bidhaa za makampuni ambayo bidhaa zake hazina ubora na kiwango kinachotakiwa.

Alisema, katika hilo ni vyema serikali wakalivalia njuga suala la bidhaa feki yakiwemo majenereta, na kampuni yake itakuwa bega kwa bega kuunga mkono juhudi zote za kuwafichua wafanyabiashara watakaojihusisha na kuingiza nchini bidhaa feki vikiwemo vifaa vya umeme.

Hata hivyo, uchunguzi wa kina unaonyesha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa hizo waliwahi kukamatwa na polisi mwanzoni mwa mwaka huu na wakakiri kutorudia mchezo huo wa "kuchakachua" bidhaa hizo, ingawa haifahamiki kwanini hawakufikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment