KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, December 15, 2010

Mgao wa umeme haueleweki


MBALI na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutangaza kusitisha mgawo wa umeme nchini kufuatia kuongezeka kwa vyanzo vinavyozalisha umeme yakiwemo maji katika mabwawa mbalimbali ya kuzalisha umeme huo, hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya maeneo ya ji
Wakazi wa jiji wakiwemo maeneo ya Ilala, Vingunguti, Buza, Kigogo, Mwenge. Mikocheni. Tandika, Kinondoni ,Tabata, na kwingineko wamekuwa wakilalamikia kukosa umeme na kushangazwa na hali hiyo kwa kuwa shirika hilo lilishasitisha mgao huo.

Wakazi hao waliokuwa wakilalamikka kwenye vyombo vya habari na kudai kuwa wanakosa umeme kwa masaa yasiyozidi mawili na siku nyingine kukosa umeme karibia siku nzima na kushangazwa na hali hiyo.

Tanesco ilitangaza kusitisha mgao huo na kudai mitambo ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imeanza kuzalisha umeme megawati 70 kwa siku.

Katika hali ya kushangaza , Meneja wa Mawasiliano wa shirika la Tanesco, Bi. Badra Masoud, alipoatakiwa kuelezea kuhusiana na kadhia hiyo ya kukatika kwa umeme katika maeneo mengi ya jiji alisema hana taarifa kama mgawo wa umeme unaendelea

No comments:

Post a Comment