KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Marufuku disko toto -Tabora


JESHI la Polisi mkoani Tabora, limewatahadharisha wenye kumbi za starehe waachane na maandalizi ya kuandaa disko kwa ajili ya watoto maarufu kama “disko toto” wakti wa sikukuu za Krissmas na mwaka mpya.


Rai hiyo imetolewa na jeshi hilo baada ya mkoa huo kupoteza watoto 19 miaka miwili iliyopita wakati wa sherehe za sikukuu ya Idd el Fitri.

Hivyo kufuatia hali hiyo Polisi wa Mkoani humo, wamepiga marufuku disko toto wakati wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

” Ni marufuku kwa wamiliki wa kumbi za starehe kuandaa mabango na kutoa matangazo kwa ajili ya disko toto kwenye zikukuu hizo, na atakayekiuka atakiona, ikiwemo na kufungliwa mashitaka mahakamani” ilismea amri hiyo ya polisi.

Hata hivyo katika kuonyesha jambo hilo linafatwa kiumakini, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, bw.Liberatus Barow amesema kuwa, jeshi hilo limejipanga vilivyo kuhakikisha kumbi hizo zinalindwa wakati wa mikesha na sikukuu zenyewe.

No comments:

Post a Comment