KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Marseille na Chelsea kuumana uwanjani leo



Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Didier Drogba wa Chelsea atarajiwa kutamba leoKatika kundi G kwenye kinyang´anyiro cha ligi ya mabingwa barani Ulaya, Real Madrid inavaana na Auxerre ya Ufaransa inayoburura mkia

Vumbi litatibuliwa leo usiku katika michuano ya kuwania nafasi ya kuingia katika duru ya kabla ya robo fainali ya kombe la vilabu bingwa, kati ya timu za Kundi E mpaka H.

Kati ya makundi hayo manne,moja tuu kundi H linalozijumuisha Arsenal ya Uengereza,Partizan Belgrade ya Serbia, Shakhtar Donesk ya Ukraine na Braga ya Ureno ndilo ambalo bado haijulikani timu gani itasonga mbele.Shakhar Donestsk inaongoza kwa pointi 12 na kuzipita kwa pointi tatu Arsenal na Braga. Mabingwa wa ligi kuu ya Ukraine wakitoka sare tuu na Ureno nyumbani,watapata nafasi ya kuingia duru zijazo ingawa hata wakishindwa haitamaanisha moja kwa moja watapigwa kumbo.

Pindi Arsenal kwa upande wake wakishinda nyumbani dhidi ya Partizan Belgrade, timu zote hizo tatu zitajikuta na pointi sawa na hapo wingi wa magoli utaamua ipi isonge mbele. Arsenal iliyowahi kuishinda sita sifuri Braga na tano moja Shakhtar Donetsk itanyakua usukani huku Braga ikilazimika kushinda kwa manne nchini Ukraine ili kuweza kusonga mbele.

Katika Kundi E linaloongozwa na Bayern Munich kwa pointi 12,watoto wa As Roma watakwenda Rumania kupimana nguvu na Cluj ili kuweza kujinyakulia pointi wanayoihitaji kuweza kuingia duru zijazo.Kwa upande wake kocha wa Bayern Munich Louis van Gaal anataraji pambano la leo dhidi ya Bâle ya Uswisi litairejeshea imani timu yake baada ya kutandikwa mawili kwa bila na Schalke 04 katika michuano ya ligi kuu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika kundi F, leo usiku mafahali wawili-Marseille na Chelsea wanateremka uwanjani katika mji wa mwambao wa Ufaransa. The Blues na Les Marseillais wote wawili wameshanyakua tikiti ya kuingia duru zijazo. Lakini pambano hili la leo lina ladha ya aina yake kwa Drogba na wakaazi wotev wa mji huo wa mwambao wa ufaransa-mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Côte d'ivoire anarejea tena katika uwanja wa Vélodrome, miaka sita baada ya kuupa kisogo na kuelekea London.

Na hatimaye katika kundi G Real Madrid inayoongoza kundi hilo itamenyana na Auxerre ya Ufaransa inayoburura mkia. Ajax Amsterdam inakwenda Milan Italy. AC Milan wameshajihakikishia nafasi ya kusonga mbele pamoja na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment