KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Maiti yakutwa kwenye lifti -Dar


MWANAUME mmoja [40-45] jina lake halikuweza kufahamika mara moja, amekutwa amekufa katika lifti ya jengo la Posta House lililopo maeneo ya katikati ya jiji.

Maiti ya mwanaume ilikutwa chini ya lifti ya jengo hilo na uchunguzi ulibaini alikufa siku tatu nyuma na alifundulika baada ya wafanyakazi wafanyao kazi aktika jengo hilo kusikia harufu kali na hawakutambua ilikuwa ikitokea wapi.

Taarifa zilifikishwa katika kikosa cha ukoaji zimamoto Kampuni ya Altimeti kwa kushirikiano na kikosi cha zimamoto wilaya ya Temeke kilifika eneo hilo kutoa maiti hiyo.

Zoezi hilo lilionekana kuwa gumu kidogo kwa kuwa waokoaji hao walilazika kuzama chini ya lifti hiyo huku wakiwa na vifaa mbalimbali na mitungi ya gesi ambapo waliikuta maiti hiyo ikiwa imeharibika vibaya hadi kufikia hatua ya kutoka ngozi na kuto harufu kali.

Maiti hiyo ilichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi

No comments:

Post a Comment