KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, December 10, 2010

Mahabusu watoroka mikono mwa polisi


Waandishi Wetu
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mahabusu wanane waliokuwa wamehifadhiwa kwenye Kituo cha Polisi cha Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo wametoroka katika mazingira ya kutatanisha usiku wa kuamkia Desemba6, mwaka huu.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilidai kuwa mahabusu hao waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na kujihushisha na wizi wa kutumia silaha, walipelekwa katika kituo hicho baada ya kutolewa katika Gereza la Kigongoni kwa ajili ya kupelekwa mahakamani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absalom Mwakyoma alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa taarifa za kutoroka kwa mahabusu hao zilitolewa na mmoja wa mahabusu 16 waliobaki katika kituo hicho hicho cha polisi baada ya wenzao wanane kutoroka.
Alisema kuwa mahabusu hao walitoroka usiku wa kuamkia Desemba 6, mwaka huu na kwamba kabla ya kutoroka walivunja dirisha dogo la kituo hicho.

“Sehemu iliyovunjwa (ambayo tayari tumeshaiziba) ilikuwa na umbo kama la mstatiri,” alisema Mwakyoma.

Kwa Mujibu wa Mwakyoma, baada ya tukio hilo mmoja wa mahabusu 16 walibaki kituoni hapo wakati wenzao wakitoroka alitoa taarifa za tukio hilo kwa walinzi wa zamu ambao pia walitoa taarifa viongozi wa polisi.
Alifahamisha kuwa baada mahabusu hao kutimka kwenda kusikojulikana, jeshi hilo liliunda timu maalumu ya kufuatilia tukio hilo ambayo ilifanikiwa kumkamata mmoja wa mahabusu hao.
“Mbali na kufanya juhudi za kuwakamata mahabusu hao timu hiyo pia itachunguza kwa kina tukio hilo ili kubaini kilichosababisha watuhumiwa hao kutoroka,” alisema Mwakyoma.

Alieleza kuwa askari polisi waliokuwa zamu katika kituo hicho cha polisi siku ya tukio hilo wamekamatwa na kuwekwa mahabusu.

“Pamoja na kuwa timu iliyoundwa inaendelea na kazi ya kuwatafuta mahabusu hao, nawataka watuhumiwa hao kujisalimisha wenyewe katika kituo chochote cha polisi. Pia naomba mwananchi yeyote atakayewaona au kuwatambua watuhumiwa hao atoe taarifa polisi mapema iwezekanavyo,” alisema Mwakyoma.

Wakati Mwakyoma akitolea ufafanuzi tukio hilo, habari zilizolifikia gazeti hili zilidai kuwa mahabusu hao walifikishwa katika Kituo hicho cha Polisi cha Chalinze Desemba 4, mwaka huu lakini kutokana na chumba cha kuhifadhi watuhumiwa kituoni hapo kuwa na watu takribani 22, waliwekwa nje ya chumba hicho.
“Usiku wa kuamkia Desemba 6, mahabusu walitoroka, ilipofika asubuhi baadhi ya nondo zilizokuwa juu ya mlango wa kituo cha polisi zilikuwa zimeng’olewa bila kujua nani aliyefanya tukio lile,” zilieleza habari hizo.

Zilieleza kuwa baada ya tukio hilo askari watatu waliokuwa katika kituo cha Polisi cha Chalinze wakati mahabusu hao walikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi mkali katika Kituo cha Polisi Kibaha.
Taarifa hizo zilifafanua kuwa mara baada ya mahabusu hao kutoweka lilitokea tukio la uporaji katikati ya eneo la Chamakweza na Pingo mkoani humo, ambalo linahisiwa kuwa lilifanywa na mahabusu hao

No comments:

Post a Comment