KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, December 22, 2010

Lori laua utingo wake


MKAZI wa Arusha , Abeidi Juma (26) amefariki dunia papo hapo baada ya kukanyagwa na gari wakati akiwa amejipumzisha chini ya uvungu wa gari hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absolomo Mwakyoma alisema juzi kuwa kifo hicho kilitokea Desemba 21,mwaka huu, majira ya saa 7:00 mchana katika kijiji cha Mdaula barabara ya Chalinze/Morogoro Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mwakyoma alisema chanzo cha ajali hiyo kilitokana na marehemu Abeid ambaye alikuwa utingo wa gari aina ya Scania Lori kujipumzisha chini ya uvungu wa gari hilo na dereva wake Bakari Ramadhani (27) kuliendesha na kumkanyaga.

Alisema gari hilo aina ya Scania lori lililokuwa likiendeshwa na dereva ambaye naye pia ni mkazi wa Arusha na kumkanyaga utingo wake, Abeid lilikuwa likitokea mkoani Dar es Salaam kuelekea Ngara.

Kamanda huyo aliongeza kusema kuwa baada ya gari hilo kumkanyaga Abeid alifariki dunia papo hapo.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi kwa uchunguzi wa daktari na dereva amekamatwa.

No comments:

Post a Comment