KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

Liu Xiabo apata tuzo ya amani ya Nobel

Kosa lake ni kupigania demokrasia kama raia

Katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu wa Norway kumtunukia mfungwa wa Uchina, Liu Xiaobo tuzo ya amani ya Nobel, mwenyekiti wa kamati inayohusika na tuzo hiyo, amesema uhusiano kati ya amani na haki za binadamu unaeleweka wazi, na hamna ubishi katika hilo.

Huku akishangiliwa mno, Thorbjorn Jagland amesema kosa la Bw Liu ni kuelezea wazi msimamo wake kama raia katika kutaka demokrasia, na ni lazima aachichiliwe huru.

Kulikuwa na kiti kitupu katika sherehe hiyo kwa kumheshimu Liu, ambaye Uchina ilikataa asafiri hadi Oslo kupokea tuzo.

Mke wake na jamaa zake wengine pia walikatazwa kusafiri hadi Uchina kupokea tuzo hiyo kwa niaba yake.

Wakati sherehe ilipokuwa ikiendelea moja kwa moja, matangazo ya kimataifa ya sherehe hiyo yalizuiliwa na Uchina, ikiwa ni pamoja na habari za kimataifa za BBC na CNN.

Vyombo vya habari vya Uchina havikuitangaza sherehe hiyo.

Tovuti nyingi pia zilizuiliwa kutangaza sherehe.

Serikali ya Uchina imeendelea kuwanyanyasa wale ambao wamekuwa wakishirikiana na Liu katika kutetea suala la demokrasia nchini humo

No comments:

Post a Comment