KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Kituko! washitakiwa wavua nguo mahakamani


KATIKA hali yakushangaza jana washitakiwa watatu katika kesi ya unyanga’nyi wa kutumia silaha, wamefanya kioja cha kufungia mwaka kwa kuchukua maamuzi ya kuvua nguo kupinga hukumu iliyotolewa mahakamani hapo.
Kituko hicho kilitokea jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dare s Salaam majira ya mchana.

Washitakiwa hao ambao ni Samuel Joseph, Saidi Idd na Said Zakaria walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha kesi ambayo ilikuwa ikiendeshwa mahakamani hapo yenye namba 184 ya mwaka 2010.

Hakimu Mkazi Ritha Tarimo aliwaachia huru washitakiwa hao majira ya saa 6 mchana kupitia kifungu namba 225[4] cha sheria ya mwenendo ya makosa ya jinai ya mwaka 1985 kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 baada ya wakili wa serikali Leornad Chalo kudai upande wa mashitaka hawakuwa na jalada la polisi la kesi hiyo.

Hivyo hakimu huyo aliwaachia huru washitakiwa hao na punde tu hakimu aliamuru kukamatwa kwa washitakiwa hao na kurudishwa mahakamani kitendo ambacho washitakiwa hao hawakuafiki kwa muda huo kupinga kukamatwa tena huku akipiga kelele waachiwe.

Kufuatia hali hiyo askari polisi walitumia nguvu za ziada washitakwia hao kuwakamata na washitakiwa hao walichukua uamuzi wa kuvua nguo zao kupinga hukumu hiyo na hata askari polisi walipowataka wavae nguo waligoma na askari kwuafikisha mahakamani humo wakiwa vivyohivyo utupu kama walivyozaliwa.


Awali washitakiwa hao walifikishwa mahakamani kwa hati ya mashtaka iliyodai kuwa, mnamo Juni 4 mwaka huu, majira ya saa 9:00 jioni wakiwa maeneo ya Mchikichini jijini Dar es Salaam, waliiba vitu mbalimbali zikiwemo simu mbili za mkononi aina ya Samsung na Nokia pamoja na nyaraka mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya Sh.467,000 mali ya David Mkombozi na kabla ya kufanya wizi huo walidaiwa kumjeruhi mwenye mali hizo kwa kumkatakata na panga kichwani li waweze kujinyakulia mali hizo

No comments:

Post a Comment