KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Jela kwa kushambulia wachezaji wa Togo

..
Mahakama moja nchini Angola imemhukumu kwenda jela miaka 24 mtuhumiwa wa shambulio la timu ya taifa ya soka ta Togo, mwezi Januari

Cabinda


Mtuhumiwa huyo ni Joao Antonio Puati. Wakili wa mtuhumiwa huyo ameliambia shirika la habari la AFP kuwa alikutwa na hatia ya kufanya "uasi kwa kutumia silaha".

Basi lililokuwa limebeba timu hiyo, lilishambuliwa katika jimbo la Cabinda, wakati wachezaji hao wakielekea katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.



Emmanuel Adebayor akipozwa na mchezaji mwenzake


Wamesema ushahidi wa uhusiano na kundi la Flec haukuoneshwa wakati kesi ikiendeshwa, bali ulitokana na taarifa za polisi zilizochukuliwa kutoka kwa Puati wakati akiwa kizuizini.

Wakili wa utetezi Arao Tempo ameiambia BBC kuwa mteja wake aliteswa wakati akiwa jela la kulazimishwa kukiri kuwa anahusiana na Flec.

Kisiasa

Amesema uamuzi wa kumhukumu Bw Puati ambaye ni raia wa Kongo-Brazzaville, na kumuachilia huru mtuhumiwa mwenzake ambaye ni raia wa Angola, ni wa kisiasa.

Amesema hukumu hiyo ni kupeleka ujumbe Kongo-Brazzaville, ambako waasi wengi na wafuasi wa Flec wanaishi na kufanya shughuli zao.

Gerezani

Wiki iliyopita, wanaharakati wanne wa haki za binaadam waliokamatwa kuhusiana na shambulio hilo la mwezi Januari, waliachiliwa huru kutoka gerezani.

Makundi ya haki za binnadam yameituhumu Angola kwa kutumia shambulio dhidi ya timu ya Togo, ili kuhalalisha msako dhidi ya wakosoaji wa serikali katika jimbo la Cabinda.

Flec imekuwa ikipigana kwa miongo mitatu kudai uhuru wa Cabinda, eneo ambalo linatenganishwa na Angola kwa kipande kidogo cha ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Licha ya eneo hilo kuwa na utajiri wa mafuta, ni moja ya maeneo masikini zaidi nchini Angola

No comments:

Post a Comment